Waume wa Uswazi na vifo vya Mapema


Hili ni jambo ambalo nimelishuhudia zaidi ya maeneo matano lakini nimeambiwa pia kuhusu maeneo mengine ya Uswazi nako ni hivyo hivyo.
Ni kwamba asilimia 80 ya maeneo mengi ya Uswazi wanawake wengi ni wajane,yaani wengi wa akina mama wanaoishi maeneo hayo wamefiwa na waume zao.
Hii ina maana kuwa ukikutana na wanawake 10 kati ya 8 waliowahi kuolewa kwenye maeneo mengi ya Uswazi ni wajane.
Lakini wanaume wanaoonekana kufariki ni wale waliofanikiwa kupata mafanikio kidogo.Karibu wote waliofariki walikua wana nyumba na biashara zingine kidogo kama maduka yale ya rejareja n.k.
Mfano,Mtaa ninaoishi una nyumba 25,20 kati ya hizo wanaozimiliki ni wanawake wajane,yaani wamefiwa na waume zao.
Nilikokua naishi siku za nyuma nako ni hivyo hivyo,wengi ni wamama ni wajane.
Kwanini?
Kwanini waume wa maeneo hayo hufa mapema?
Na ni kwanini wanaofariki wote hali zao za kimaisha zinafanana?Yaani wale walio na hali za chini kabisa wapo na wake zao mpaka wengine wamezeeka.
Kwanini?
Mimi sina jibu la moja kwa moja labda wewe unaweza kunisaidia!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad