WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud,
amechafua hali ya hewa wakati wa mazishi ya Padri Evaristus Mushi,
aliyeuawa kwa kupigwa risasi Visiwani Zanzibar.
Hali hiyo iliyosababisha waziri huyo azomewe, ilitokea jana kwenye
mazishi ya padri huyo, yaliyofanyika katika makaburi ya watawa, yaliyopo
eneo la Kitope, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mbele ya Rais wa SMZ, Ali Mohamed Shein, Waziri huyo aliwachefua
maelfu ya Wakristo waliofurika kwenye mazishi hayo wakati akitoa salamu
za pole kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Katika salamu hizo, waziri huyo alianza vizuri kwa kutoa pole na
kwamba serikali imeguswa na kifo hicho na maumivu waliyonayo waumini
ndiyo iliyonayo pia serikali.
Lakini wakati akiendelea kutoa salamu hizo, alichafua hali ya hewa kwa
kusema kifo cha Padri Mushi kimetokana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
“Ndugu zangu poleni kwa msiba huu, serikali imeguswa sana na kifo
hicho kama ndugu na waumini mlivyoguswa. Hata hivyo hii ni mipango na
mapenzi ya Mwenyezi Mungu…”
Kauli hiyo ilisababisha umati wa watu waliofurika katika makaburi hayo
kupaza sauti kwa kuzomea na kuikejeli Serikali ya SMZ kwamba kifo hicho
hakikutokana na mapenzi ya Mungu.
Katika zogo hilo, wapo waliopaza sauti kwa kusema kifo hicho
hakikutokana na mapenzi ya Mungu, kwani hakufa kwa ajali ya maji, ajali
ya gari wala kugongwa na gari.
“Hatutaki kusikia hilo, Padri Mushi hakufa kwa mapenzi ya Mungu.
Hatutaki kusikia… huo…” zilisikika sauti za baadhi ya watu waliohudhuria
mazishi hayo.
Wakati zogo hilo linaendelea, Waziri Aboud alishindwa kuendelea kutoa
salamu hizo, hali iliyosababisha Askofu wa Jimbo la Zanzibar, Dk.
Augustino Shao kuingilia kati.
Shao aliungana na waumini kwa kusema kifo cha Padri Mushi hakikutokana
na mapenzi ya Mungu bali kimetokana na magaidi waliokatiza uhai wake.
Kauli hiyo iliibua kelele za shangwe kutoka kwa waumini hao ambao waliendeleza kelele za kumzomea Waziri Aboud.
Askofu Shao alisema wakati huu si wa kukumbatia maovu na kusisitiza
kifo cha Padri Mushi hakikutokana na mapenzi ya Mungu, bali kimefanywa
na watu wakatili waliokatiza maisha yake.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa wakati akitoa salamu za chama chake, alisema kuwa taifa
liko katika hatari ya kusambaratika kwani kuna viashiria vya wazi
vinavyoonesha kuwa tuko katika wakati mgumu.
Alivitaja viashiria hivyo kuwa ni pamoja na kuuawa kwa kupigwa risasi
Padri Mushi, kupigwa risasi kwa Padri Ambrose Mkenda, kuuawa kwa
mchungaji Geita katika mzozo wa kuchinja, kuuawa kwa mwandishi wa
habari, Daudi Mwangosi na matukio mengine.
Dk. Slaa alitofautiana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kuleta
wachunguzi kutoka nje, akisema hatua hiyo ni sawa na kushughulikia tawi
badala ya kukata shina na mizizi.
Mbali ya matukio hayo, ibada ya kumuaga padri Mushi ilianza saa mbili
asubuhi na kufanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, katika eneo la
Minara Miwili mjini hapa.
Hao ni waumin ambao bado wanachuki na kutaka kuendeeza mapambano dhidi ya uislam na dhani yatatokea mengi juu ya hilo visiwani zanzibar ye2 macho 2shuudie vita
ReplyDeleteWaziri hakukosea kwamba kifo cha padri ni mapenzi ya mungu. Hakuna hata andiko ktk kitabu chochote cha dini kilichosema mtu akifa kwa maji,moto,ajali ya gari/ndege na kadhalika bac ni mapenzi ya mungu. Bali mungu anasema siku ikifika utakufa tu bila kuangalia aina ya kifo.
ReplyDeleteInamaana hawaamini km kuna Mungu na kila ki2 kinatokana na mapenzi na mipango yake?
ReplyDeleteInamaana hawaamini km kuna Mungu na kila ki2 kinatokana na mapenzi na mipango yake?
ReplyDeletewatu wengne wapuuz tu..mnakoment ujinga uliopo vchwan mwenu.
ReplyDeleteMpuuz ni anaesema mungu hajapanga kifo hicho!
ReplyDeletekwann mapadri tu na si mashehe ?
ReplyDeletekweli nyinyi hamuna dini hivi kuna kitu kufanyikacho bila ya mapenz ya Mungu na yy ndio apangae kila aina ya kifo cha mtu na sio bina adamu huo ni sababu tu
ReplyDelete