Yule Tapeli wa Ajira za Kazi Akamatwa Baada ya Kuwaliza Wengi
1
February 23, 2013
BAADA ya watanzania wa kada mbali mbali kutapeliwa kwa njia mbali mbali hasa kupitia mawasiliano ya simu hatmaye mtuhumiwa mkuu wa vitendo vya utapeli nchini ambae anamiliki majina zaidi ya matatu kwa kutapelia watu amekamatwa jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa huyo ambae anamiliki majina zaidi ya matano amekuwa akitapeli watu wa kada mbali mbali wakiwemo wanahabari, walimu na hata wafanyakazi wa Hoteli na watu wengine wengi leo amekamatwa eneo la Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam baada ya mtego kabambe uliowekwa na mmoja kati ya wanawake waliotapeliwa ambae ni mfanyakazi wa Hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa)
Mfanyakazi huyo wa Hoteli ameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo kuwa yapata siku mbili zilizopita tapeli huyo ambae alijitambulisha kwa jina la Kevin alimpigia simu na kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwalimu wake wa chuo cha Hoteli na utalii kama anatafuta kazi nje ya Hoteli hiyo hivyo yeye ni meneja wa Hoteli ya Flamingo hivyo yupo tayari kumpa ajira katika Hoteli hiyo na kama anaowezake kama watano awaeleze kuwa nafasi ipo.
Imedaiwa kuwa Kevin kama alivyojiita katika utapeli huo baada ya dakika chache alimpigia tena simu mwanamke huyo na kumtaka siku ya pili wakutane katika Hoteli hiyo ya Flamingo ili awaonyeshe mazingira ya Hoteli hiyo na kujua nini cha kufanya .
Hata hivyo mara baada ya kufika siku iliyopangwa kama walivyoahidiwa aliwataka kila mmoja kutoa fedha kiasi cha shilingi 30,000 kwa ajili ya kushonewa sare za Hoteli hiyo sare ambazo zingekuwa ni mali yao kutokana na wafanyakazi wengi kuwa na tabia ya kukimbia na sare sasa wameamua kila anayefika kuomba kazi awe na sare yake toka nyumbani kwake.
Alisema kuwa baada ya kutoka kiasi hicho cha fedha yeye pamoja na mwenzake mmoja tapeli huyo aliwataka kukaa nje ya Hoteli hiyo ili afanye mawasiliano na mkurugenzi ndipo awaite ofisini na baada ya hapo kweli aliingia ofisini ila jinsi alivyotoka haikufahamika na wao kujikuta wanakaa hadi saa 12 za jioni bila mtu kuonekana na kuamua kuuliza kwa wahusika na ndipo walipobaini kutapeliwa baada ya kuambiwa hakuna ajira mpya zilizotangazwa hapo na kuwapa utaratibu wa ajira unavyotumika kutangazwa katika Hoteli hiyo.
Kutokana na kulizwa kiasi hicho cha pesa kitu cha 60,000 kwa wawili ndipo usiku alipompigia simu tapeli huyo na kujifanya akiulizia majibu kwa madai kuwa jana alipatwa na msiba hivyo aliondoka mapema zaidi .
"Kweli baada ya kumpigia simu tapeli alionekana kuwa mkali zaidi kuwa ni mambo gani nimefanya yeye alitoka kujua kutufuata hakukututa hivyo akataka kujua lini nitakuwa tayari kufika ili nianze kazi...na ndipo nilipomwomba nafasi yangu nimpe mtu mwingine mimi nilidanganya kuwa nitachelewa kurudi ....ila bila kujua nilikuwa namtega alikubali na kusema nimpe namba za huyoa atakayechukua nafasi yangu na wengine wawili kama wapo...na hapo ndipo nilipoweka mtego na leo tumemkamata"
Tapeli huyo amekuwa akijiita majina mbali mbali likiwemo la Abdalah Mkwachu, Aman kwa namba hizi 0713094986,07162404425
Pia inadaiwa ndie aliyepata kutapeli watu kupitia ajira hewa za TGNP kwa kutumia jina la Lilian Dihalo, mwenye namba za simu 0717-196386 ila pia inasadikika ndie aliyewaliza wanahabari wengi nchini kupitia jina la Zuhura Kambangwa.
Mbali ya makundi hayo tapeli huyo anadaiwa kuwatapeli walimu na watu mbali mbali maarufu nchini kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.
Duh
ReplyDelete