Ay Asema "Mimi ni Bonge la Mwigizaji"

MSANII wa Bongo fleva ambaye alifanya vizuri katika filamu ya Girlfriend mwanzoni mwa miaka ya 2000, Ambwene Yesaya ’AY’ amefunguka kwamba yeye ni bonge la mwigizaji wa filamu na akiingia  moja kwa moja kwenye tasnia hiyo atawafunika wasanii kibao wanaoigiza hivi sasa.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, AY amesema kwa sasa ana mambo mengi yanayomfanya ashindwe kuigiza lakini kama kuna mwandaaji wa filamu akimuhitaji afanye muvi, basi ajipange na awe na mkwanja mrefu wa kumpa.
“Nilipanga kuandaa muvi na  (Hamis) Mwinjuma ‘MwanaFA’ lakini mambo yamekuwa mengi ila dhamira ipo palepale kama muda ukipatikana tutafanya muvi wadau wangu wakae mkao wa kula,” alisema.
Pamoja na hayo, Ay aliongeza kuwa kati ya wasanii anaowakubali katika tasnia hiyo ni Irene Uwoya kwani anafanya filamu kwa uhalisia.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hakuna msanii bongo anaehustle ka wewe..uko leve nyingine..big up

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad