Wasanii wa kizazi kipya [Bongo Flava] bado wamekuwa wakilalamika kuibiwa mapato kama sio kazi zao bila ruhusa zao.
Mapato hayo ambayo yako katika mfumo wa miito ya simu, yaani caller tunes wameonekana kutokushiriki kwenye mauzo haya na wengine wameonekana kulalamika moja kwa moja kupitia mitandao ya jamii.
Earlier today, msanii anaefanya vizuri sasa na ngoma zake tofauti, akifanya muziki wa RnB, Rama Dee ameandika katika ukurasa wake wa twitter akilalamikia wimbo wake kuuzwa bila ridhaa yake.
Hii inaonesha kutokuwemo kwa makubaliano ya kuuzwa kwa KUWA NA SUBIRA.
Msanii mwingine alieonekana kuwa na matatizo kama haya Ben Pol, msanii mkali wa RnB kutoka Bongo akiwa na credit nyingi kutokanana na kazi zake nzuri.
Ben pia ameonekana leo kulalamikia suala hili hili akionekana kuhuzunika na kuwa na hasira juu ya hili,
Nafikiri hili ni tatizo linalowasumbua wasanii wengi ingawa hawa ni wachache waliolalamika leo, as fans we wanna see these guys win na kutengenza pesa zao kwa jasho wanalolitoa kwa kazi zao.
So far, suala la caller tunes limekuwa na cnflicts na wasanii wengi huku wengi wao wakidai kuwemo lakini bila ya kupata mapene yoyote au kutopata kabisa kutoka huko kwenye makampuni haya.