Demu wa Mwinyi wa Machozi Band:Madawa ya Kulevya yalitaka Kuniua


Mwanamitindo wa Bongo, Nesha Mfinanga ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji wa Bendi ya Machozi, Mwinyi Ahmed, ameeleza jinsi madawa ya kulevya yalivyotaka kuharibu maisha yake.
Akizungumza na Ijumaa kwenye kituo cha kutibia mateja cha Pilli Missana Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar, Nesha alisema mwanzo alikuwa msichana safi aliyekuwa akijipenda lakini ghafla akajikuta kwenye ulevi huo na kuharibika.

Nesha afunguka
Akizungumzia jinsi alivyoanza ulevi huo, mrembo huyo alidai kuwa, alipata msukumo kutoka kwa mpenzi wake na hata yeye (huyo mpenzi wake) alikuwa akitumia.
“Nilikuwa na maisha mabaya sana kutokana na uvutaji wa unga. Aliyesababisha niingie huko ni mpenzi wangu ila nashukuru nimekuja hapa, nimetibiwa na sasa niko safi. Nimerudi kuwa mrembo.
“Nawashauri sana wasichana wenzangu kuwa makini na wapenzi wao, hasa hawa mastaa maana usipojiangalia unaweza kuharibikiwa hivihivi unajiona.”

Mwinyi ahusishwa
Kumekuwepo na madai kuwa, mrembo huyo alijiingiza kwenye utumiaji wa madawa hayo baada ya kuwa kwenye uhusiano na Mwinyi na inadaiwa ndugu wa Nesha waliwahi kumpiga msanii huyo wakimtuhumu kumharibu binti yao.
Mwinyi anazungumziaje madai hayo? Msikie kwenye mahojiano haya hapa chini;
Ijumaa: Kuna madai kuwa Nesha alikuwa ni mpenzi wako na wewe ndiye uliyemfundisha uteja, unalizungumziaje hili?
Mwinyi: Kwa kweli hayo madai si kweli, Nesha sikatai alikuwa demu wangu licha ya kwamba nina mchumba anayeishi Sweden. Hilo la kumvutisha unga si kweli. Namfahamu ambaye alikuwa anampa kilevi hicho, anaitwa Zahir.
Ijumaa: Mbona inadaiwa wewe ndiye uliyemuingiza huko na mpaka ikatokea ndugu zake kukupiga kwa madai ya kumharibu binti yao?
Mwinyi: Kweli, nakumbuka ilikuwa mwaka jana, mwezi wa 12 kwenye msiba wa mama wa Nesha kule Kiwalani. Nikiwa pale msibani baadhi ya ndugu zake walinivamia na kunipiga hadi nikazimia kwa madai hayo, nilikwenda kuripoti polisi na kesi ipo.
Ijumaa: Lakini inasemekana hata wewe mwenyewe unatumia kilevi hicho, funguka.
Mwinyi: Siyo kweli, niko tayari hata kwenda kupima, sitaki kuchafuka kwa skendo hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad