NCHI za wenzetu staa kupiga picha za utupu si kitu kigeni lakini Kibongobongo sheria na maadili ya Mtanzania hayaruhusu kufanya hivyo.
Licha ya kubanwa na sheria pamoja na maadili, wapo wasanii ambao kwa nyakati tofauti walijikuta katika adha ya kupigwa kama si kujipiga picha za utupu kisha zikazagaa mitaani.
Wapo waliotajwa kupiga picha hizo kwa kusaka umaarufu, waliopigwa na wapenzi wao kisha wakazivujisha lakini wengine imedaiwa kuwa wamezivujisha wenyewe na kusingizia zimevujishwa na wapenzi wao.
Ifuatayo ni orodha ya wasanii mbalimbali Bongo ambao waliwahi kukwaa skendo ya picha za utupu:
Wema Sepetu:
Mwaka 2010 picha yake ya utupu ilizagaa mtandaoni huku ikidaiwa kuwa chanzo cha kusambaa kwake ni boifrendi wake ambaye alimpiga na kuzisambaza. Kama hiyo haitoshi, mwaka huu mrembo huyo alidaiwa kuposti picha zake nyingine za utupu katika mtandao wa Instagram.
Diana Hussein:
Huyu ni Miss Dar Indian Ocean ambaye pia ni Miss Kinondoni namba 2 mwaka jana, mrembo huyo hivi karibuni amejikuta akipata aibu baada ya picha yake ya utupu kuvuja. Ilidaiwa kuwa alifanya hivyo kwa azma ya kusaka umaarufu.
Jack wa Chuz:
Ni bonge la ‘actress’ Bongo Movie, mwaka 2012 alipigwa picha za utupu na kusambazwa kila kona ya Jiji la Dar. Ilidaiwa kuwa kuna mtu alizichukua picha hizo kutoka kwenye simu yake na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari.
Agness Masogange:
Nini picha! Yeye ilivuja video yake ya utupu kabisa. Ilisambaa kama njugu katika mitandao ya kijamii mwaka jana. Vyanzo makini vilidai kuwa video hiyo alipigwa na mpenzi wake na haikujulikana mara moja chanzo kilichozivujisha.
Marry John:
Msanii wa filamu Bongo, Mary John ‘Maua’ mwaka jana alijipatia jina baada ya kupiga picha kadhaa za utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii yeye mwenyewe.
Aunt Lulu:
Mara kadhaa amekuwa akitengeneza vichwa vya habari magazetini kwa kupiga picha za utupu. Mfano hai ni picha ambazo alipiga mwaka jana, ambapo alidai kuwa alipigwa bichi alipokwenda ‘kula bata’.
Lulu:
Mwaka 2010 alijikuta akichafuka kwa kutajwa kwenye skendo ya kupiga picha ya utupu. Alipoulizwa kuhusiana na picha hiyo alikanusha kuwa si ya kwake na kudai kuwa ilitengenezwa na watu ili kumchafua.
Jack Patrick
Kwa upande wake suala la kuvuja kwa picha zake za utupu siyo ishu. Mwaka jana ilidaiwa kuwa aliziposti picha zake za utupu kwenye mtandao wa BBM, haileweki ni kwa nini huwa anafanya hivyo.
Isabela ‘Vai wa Ukweli’:
Huyu ni chipukizi kwenye anga la filamu Bongo, mara kadhaa amepigwa picha za utupu na kusambazwa kwenye vyombo vya habari. Imedaiwa kuwa hufanya hivyo kama kutafuta mlango wa kutokea kwenye ustaa.
Maadili ya Mtanzania yanatukataza kufanya vitendo vya namna hii hivyo ni vyema wahusika wakawa makini, waepuke kupiga wala kuhusika kusambaza picha zao za utupu kwa namna yoyote ile.
Source:Global Publisher
weweee waache waweke sie tuburudike tu kwan hawaoni wanajidhalilisha
ReplyDeleteDuh hawa wasani sasa wanatuchosha nadhani vyama vya wasani na baraza la sanaa nchini lichukue hatua kwani huu ni uvunjifu wa madili yetu watanzania
ReplyDelete