Inawezekana Kupata Mume au mke Mzuri Kupitia Facebook?
1
March 23, 2013
Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada, sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia mitandao ya kijamii kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka kuanzisha kwani unahitaji kumfahamu zaidi na ndipo utakapoweza kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.
Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na maamuzi yako.
Ulimwengu huu wa sayansi & tekinolojia watu wengi hasa vijana wamejikuta wametekwa na mitandao ya kijamii kwa kujihusisha na mapenzi lakini ukweli unabaki kuwa palepale mandiko yanasema tumia walau miezi 6 hadi miaka miwili kumchunguza mchumba wako siyo ukurupuke mana huko ni kuingia kinyemela/kienyeji hali hiyo husababishwa na tamaa ya mapenzi.
ReplyDelete