Idadi ya matukio ya kutisha inazidi kuongezeka kwenye vichwa vya habari, naitumia post hii kutoa info za alipofikia mwigizaji Wema Sepetu kuhusu ile ishu ya kutishiwa maisha na wasiojulikana siku chache tu baada ya kufungua ofisi yake mpya na ya kisasa itakayokua inaandaa filamu za kitanzania na kazi nyingine kama hizo.
Namkariri Wema akisema “nilichokifanya nilitoa taarifa, nimekwenda kuripoti polisi kwa hiyo nawasubiria tu wanifanyie walichokua wanataka kufanya, mpaka sasa hivi sijagundua ni kina nani ila mtu alienipa ripoti za vitisho aliniambia ni watu ambao nina uhasama nao na hawapendi maendeleo yangu, akasema pia hao watu nawajua lakini hakusema kama ni waigizaji au ni kina nani ila wanataka kunivamia ili kunikomesha…. mimi sina uhasama na mtu yeyote”
Kuhusu ulinzi wake kwa sasa, Wema amesema “nyumbani nimeongeza ulinzi japo nilikua na walinzi, sikua na walinzi wenye silaha ambao sasa hivi wanakuepo, pia nimeweka alarm system kali na za kisasa…… vitu vingine ni kama kuwa makini ninapokwenda na watu ninaokuwa nao”