Tanzania haijawahi kucheza fainali za Kombe la Dunia zaidi ya kuishia hatua za awali, lakini kama mikakati ikiandaliwa kikamilifu, nafasi hiyo ipo na inaweza kufika mbali.
Kama ilivyo kwenye msimamo, Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ikiwa na pointi tatu, ikiwa ni pointi moja nyuma ya vinara hao wa pili kwa soka Afrika.
Morocco kabla ya mchezo wa kesho ina pointi mbili baada ya sare mbili wakati Gambia ni ya mwisho ikiwa na pointi moja.
Ushindi wa timu hiyo, utafufua na kutia chachu nafasi ya Tanzania kufika mbali katika fainali hizo za Kombe la Dunia kupitia Kanda ya Afrika.
Kinachotakiwa ni kwa wachezaji kucheza kwa nguvu, ari, moyo na mshikamano kuhakikisha wanashinda mchezo huo, huku kila mmoja kwa nafasi yake akiomba dua ya kheri na mafanikio kwa Taifa Stars.
Lazima Morocco washangazwe na soka ya Tanzania. Haiwezekani kila siku Nigeria, Ghana au Cameroon kama tuliwamudu Zambia na Cameroon katika mechi za kirafiki, kwa nini leo isiwe Morocco?