Kutoka Jamii Forums:FastJet Sidhani Kama Itadumu
3
March 29, 2013
Kila nikitazama huduma zinazotolewa na FastJet, sioni kama ina uhai mbele ya safari. Precision nadhani wamejiimarisha, na wana ubunifu wa kweli wa kibiashara.
FastJet wana bei nafuu kuliko Precision, lakini saikolojia ya binadamu ni ya ajabu na hii itawasaidia wapinzani wa FastJet. Ukiingia kwenyue FastJet, unalazimika kununua maji (hata kama ni ya kunywea dawa), soda, bia, kahawa au chakula chochote. Ukiwa na mzigo hadi kilo 20, ni kazima ulipe dola 5 za Marekani. Kuanzia kilo 21 na kuendelea, kila inayozidi unapaswa kulipia dola 5. Ukiwa na ka-perfume au lotion, hata kama ni mikebe miwili, unapaswa ku-check in kwa kulipia dola 5( bila kujali ukubwa au uzito wa kitu).
Wenzao Precision wanachofanya ni kwamba nauli zao ziko juu, lakini ndani ya ndege wanatoa maji, pombe, soda na vyakula japo ni vya ujanja ujanja (hasa chakula). Wanaruhusu abiria kuwa na mzigo wenye uzito wa hadi kilo 30! Hii imewafanya abiria wanaotoka Mwanza wawe na samaki wengi. Ndoo zenye samaki ndizo zinazopamba Precision. FastJet hawataki kusikia kitu "ndoo za samaki". Kwa mazingira yetu ya Kiafrika, unaona hapa Precision wana nafasi nzuri zaidi kibiashara. Kulithibitisha hili, nimeanza kuona FastJet wakianza kukosa wateja. Kwa mtazamo tu wa kawaida, sioni kama hawa jamaa watadumu kwenye soko. Kama wana madeni, TRA wafanye haraka! Hawa wanaweza kuwa kama Meridian Biao Bank! Wanaweza kutuacha kwenye mataa!!
Source: Jamii Forums
Tags
Ni wapumbavu Sanaa hao eti ukiuliza unaambiwa ndege ya mzungu Mzungu my foots!I'm one of customers ambao sitapanda hiyo ndege teenaaaa Washenzi sana mxssss
ReplyDeleteBigup Precision
Sio lazima upande iyo ndege.. Wapo wengi wataopanda bcz sio kila mtu anauwezo wakununua ticket ya precision!
ReplyDeleteKwani unalazimishwa, c unataka mwenyewe!? Km unaona ni ghali sn, kuna mabasi kibao yapo stendi
ReplyDelete