Madenti wa Kike Udom Wasema:Wabunge ni Mabuzi Yetu Huku



MITANDAO mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Unyemeleaji taarifa uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya kisasa  umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’ baadhi ya wabunge.

Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa umma.
 
SIKILIZA TUKUPASHE
“Shoga naona unawapanga tu waheshimiwa,” mchangiaji mmoja kupitia kundi la BBM alichangia kwenye moja ya picha aliyoweka rafiki yake akiwa amepozi na mbunge mmoja kutoka mikoa ya Magharibi  (jina kapuni) ambapo bila haya majibu ya mwenye ukarasa huo yalikuwa: “Maisha bila mabuzi hayaendi bi dada.”

Upekuzi wa kiintelijensia wa Ijumaa ulichungulia dokezo za wachangia mada na kubaini kuwa waheshimiwa wanaoingia mjengoni kama wawakilishi wa wananchi wanachukuliwa kama mabuzi kwa tafsiri ya kuchunwa fedha huku kipindi cha vikao vya bunge vikichukuliwa kama nyakati za migodi kutema dhahabu.

MAMBO YA KUFEDHEHESHA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wasichana hao wa chuo wamekuwa wakihifadhi picha za utupu za wabunge wenye uhusiano nao kwenye simu zao za mikononi walizowapiga walipokuwa wakifanya nao ngono ambapo wakati mwingine huzitundika mitandaoni kwa kubipu na kuziondoa haraka lengo likiwa ni kuwaonesha ushahidi huo marafiki zao.

Miongoni wa wabunge waliokumbwa na aibu hiyo ambao Ijumaa liliziona picha zake za aibu ni pamoja na mbunge anayetoka kanda ya Kusini, mwingine kanda ya ziwa na mmoja kutoka jijini Dar es Salaam huku waziri mwenye heshima kubwa naye akiingia mkenge kwa kupiga picha na msichana wakiwa kitandani vifua wazi.

WANAFUNZI WA KIUME WANASEMAJE?
Ijumaa lilipowauliza baadhi ya wanafunzi wavulana wanaosoma chuoni hapo juu ya kuwepo kwa tabia za  baadhi ya wabunge kutembea na wanafunzi wa kike walikiri na kuongeza kuwa ukata ndiyo unaosababisha baadhi ya wanachuo wajitongozeshe kwa waheshimiwa.

“Wanachofuata ni fedha siyo mapenzi, wapo wasichana hapa kipindi cha bunge hawaonekani kabisa chuoni, wanakuwa na waheshimiwa wakistarehe, kuna wengine wanasomeshwa, wanahudumiwa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonny.

IJUMAA LINASEMAJE?
Dawati la Ijumaa linawatahadharisha waheshimiwa wabunge wenye tabia za ukware kuachana na mambo ya kihuni, badala yake wajiheshimu vinginevyo watajikuta matatizoni na kuambulia aibu kubwa mbele ya jamii kwa kuanikwa kwenye magazeti siku si nyingi pia picha zao za aibu zitafikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

RIPOTI IMEANDIKWA NA  GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Viongozi walikuwepo zamani, na sio hawa wanaojibatiza majina ya Dk. au Mheshimiwa. Enzi za Ndugu ndio tulikuwa na angalau unaweza kuuita uongozi.

    ReplyDelete
  2. Viongozi walikuwepo zamani, na sio hawa wanaojibatiza majina ya Dk. au Mheshimiwa. Enzi za Ndugu ndio tulikuwa na angalau unaweza kuuita uongozi.

    ReplyDelete
  3. hakuna jipya.
    Tushazoea dadadeq

    ReplyDelete
  4. hakuna jipya.
    Tushazoea dadadeq

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad