Mbwa Watumika Kutuliza wafuasi wa Chadema Jana Baada ya Lwakatare Kurudishwa Rumande
0
March 21, 2013
Jana asubuhi mbwa wa polisi waliwatuliza wafuasi wa Chadema waliofika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Muganyizi Lwakatare. Polisi wa kikosi cha mbwa na vikosi vingine walikaa tayari kuwadhibiti wafuasi hao walioanza kupiga mbiu ya chama hicho ya "Pipooooz..." baada ya kiongozi wao kushindwa kutolewa kwa dhamana. Lwakatare amerudishwa tena rumande baada ya kufutiwa mashitaka yake yote yanayomkabili na baadaye kukamatwa na kurudishwa rumande. Kesi yake itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.