Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.
Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
Moshi Mweusi Wafuka Vatican_Papa Bado Hajapatikana
2
March 13, 2013
Tags
Hi, yes this piece of writing is really fastidious and I have learned lot of things from it regarding blogging.
ReplyDeletethanks.
Look at my page Medical School Application Consultant
Hi, all is going nicely here and ofcourse every one is sharing facts,
ReplyDeletethat's actually excellent, keep up writing.
My blog Bubble Butt ()