Mr Chuzi Kulikoni? Akimbiwa na Wasanii 35
0
March 24, 2013
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tuesday Entertainment Ltd, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ amekimbiwa na wasanii wake 35 ambao wamekwenda kuanzisha kundi lao jipya waliloliita Green Message Entertainment.
Meneja uzalishaji wa kundi hilo jipya, Erica Swila aliliambia gazeti hili kuwa miongoni mwa wasanii waliomkimbia Mr. Chuz ni Mustapha Kirobo aliyetunga Tamthilia ya Milosis na Red Apple na tayari kundi hilo limekamilisha tamthilia yao itwayo Green Message ambayo inarushwa katika Runinga ya TBC 2.
“Mimi na wenzangu tulioondoka kwa Mr. Chuz tumefanikiwa kucheza tamthilia yetu ya kwanza tuliyoipa jina la Green Message, tunawakaribisha wasanii wenye umri kuanzia miaka 35 na kuendelea, waje wajiunge nasi,” alisema Erica.