Mwanamke Ajitokeza na Kudai Jack wa Chuzi Kamuibia Mume

ZENGWE limeanza! saa 48 baada ya Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na jamaa aitwaye Gadna Dibibi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Omary ameibuka na kudai muoaji ni baba mtoto wake wa miezi minne hivyo anamuomba msanii huyo amwachie mumewe.

Mariam Omary anayedai Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kamchukulia baba watoto wake akiwa na mwanaye.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya kuenea kwa habari za Jack Chuz kufunga ndoa na kijana huyo wikiendi iliyopita, ndipo ilipogundulika kuwa ana mwanamke ambaye wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani miaka mitatu na wana mtoto huyo mmoja wa kiume.
Baada ya ripota wetu kuidaka ishu hiyo aliingia mzigoni kutafuta ukweli wa jambo hilo ndipo akakutana na mwanamke huyo aishie Kigogo, Dar ambapo alikutwa akiwa anambembeleza mtoto huyo anayeitwa Price Laden.
Akifunguka mbele ya paparazi wetu, Mariam alidai kwamba siku ambayo mwanaume huyo alifunga ndoa (Ijumaa), alimuaga anasafiri kwenda Morogoro hivyo hatakuwepo Dar lakini wanusaji wa mambo ya watu walishampa ‘infomesheni’ kwamba anafunga ndoa na Jack Chuz.

“Unajua mtu atakunyima ugali ila siyo maneno, nilishajua na nilikuwa namwangalia tu nione atasemaje,” alisema.
Mariam aliendelea kutiririka kwamba anamjua vizuri Jack Chuz linapokuja suala la wanaume wa wenzake lakini kwake atachemsha kwa kuwa msanii huyo anajua kila kitu juu ya uhusiano wake na mwanaume huyo ambaye ni halali yake.
“Hakuna asichokijua kati yangu na Dibibi, kwa usalama wake Jack aniachie mume wangu,” alilalama mwanamke huyo.
Baada ya kuzungumza na Mariam, mwandishi wetu alimvutia waya mume wa Jack na kusomewa mashitaka yake ambapo alisema kuwa baba wa mtoto anayemjua ni mama peke yake na isitoshe kuzaa naye isiwe sababu kwani yeye hakumuoa.
“Alikuwa demu wangu na kuzaa mtoto isiwe sababu. Hata hivyo, ukweli wa baba wa mtoto anayejua ni mama. Sikumtolea mahari wala kumvalisha pete ‘so’ hana kizuizi na ndoa yangu,” alisema jamaa huyo kisha akakata simu.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe mwanamke usijidhalilishe,huyo bwana ndie alitakiwa ajue thaman yko so usimlaum manamke mwenzio ictoshe kuzaa cyo ndoa,maisha yanaendelea fanya yako tu dada.hii ndyo dunia....

    ReplyDelete
  2. Acha umatako we mshikaji, kaa na mzazi mwenzio mlee kijana wenu.

    ReplyDelete
  3. Jack c kaolewa kiislam sasa da Maryam dini yetu inaruhusu na pia wewe hujaolewa kuzaa c kuolewa dada jichunguze kwanini kakuacha. Rekebisha makosa songa mbele utapata wa riziki yako.

    ReplyDelete
  4. We dada huna thaman tena kwake cha msingi tafuta na wew mwanaume akuoe ngoma iwe droo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad