Wasichana wadogo wafanya biashara ya ngono


Ni usiku wa saa 4 nipo katika eneo maarufu la Buguruni lililopo jijini Dar es Salaam nikiwa nimekaa napata kinywaji kwenye baa moja.


Katika eneo hilo ambalo lipo pembezoni mwa Barabara ya Mandela si tulivu sana kutokana na pilika pilika za magari na watu wanaopita karibu kwa shughuli mbalimbali.
Huku nikiendelea kupata kinywaji mara naona wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wakizunguka zunguka katika eneo hili la baa.


Awali nilifikiri walikuwa wakitafuta msaada au wakipita kuelekea nyumbani kwao, kwani umri wao haukunipa picha kwamba walikuwa kazini wakati huo wa usiku wa kiza kinene.
Kilichonifanya niwaangalie kwa udadisi zaidi ni kuona jinsi walivyovaa nguo ambazo zilionyesha nusu ya sehemu zao za mapaja, huku kifuani wakiwa wamevaa blauzi zilizobana zikionyesha matiti yao madogo ambayo yanaanza kuchipua.


Kilichonitisha zaidi ni kuona wasichana hawa ambao wakati huo walipaswa kuwa nyumbani wakiwa mkononi wameshika vinywaji vikali aina ya ‘viroba’ na wengine wakivuta sigara.
Hawa ni sehemu ndogo tu ya wasichana wadogo ambao hukesha usiku kucha katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakitafuta wateja ili wapate fedha za kujikimu.
Mwandishi analazimika kuwadadisi wasichana hawa ili kujua nini kilichosababisha waingie katika biashara hii.

Inavyokuwa
Mwandishi ana mwita mmoja wa wasichana hawa Neema Mashiri (16) (sio jina lake halisi) na kuongea naye katika sehemu tulivu katika baa hiyo huku wakitumia vinywaji kunogesha mazungumzo.


Neema akiwa mwenye kujiamini na kazi yake bila ya kutetereka anasema kazi hiyo aliianza zaidi ya miezi sita nyuma huku akiwa tayari amekutana na idadi ya wanaume ambayo haikumbuki kutokana na wingi wake.


“Kwa siku moja nakutana na wanaume katiya watano hadi saba na hii hutegemea siku na siku, kwani kuna siku huwa na biashara ya kutosha na tunapata fedha za kutosha,” anasema Neema.


Neema akieleza ujira ambao hulipwa anasema ni Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa muda usiozidi dakika 30 kwa mwanamume mmoja huku wakati kwa yule anayetaka kulala naye hadi asubuhi hutakiwa kulipa Sh10,000 hadi Sh15,000.


“Baadhi ya wanaume wamekuwa wakitufanyia vitendo vya kikatili kwa kutuingilia kinyume cha maumbile, lakini kutokana na hali ngumu ya maisha hukubali kwani dau huwa kubwa Sh10,000 hadi Sh12,000, lakini wengine hutumia ubabe tu na kututumia bila kutulipa,” anasema Neema na kuongeza;

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad