Account Ya Twitter Ya AY Yawa Verified


Account ya mtandao wa kijamii ya Twitter ya mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya yatambulika rasmi. Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.
      Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali kama muziki, serikali, siasa, uigizaji, dini, mitindo, uandishi wa habari, biashara n.k.
Ambwene Yesaya [@AyTanzania] amekuwa ni mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania mkubwa anaeendelea kufanya vizuri duniani na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika tasnia ya muziki, for his twitter account to be verified amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba [@jmakamba].

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad