Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.
Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.
Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
Nyumbani kwa mbunge hakai mbunge mwenyewe. Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke, ndugu etc. Utapigaje mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa mauaji. Lema si jambazi, ni kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana na mzalendo kwa taifa lake.
Hii wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological tortue.
Kama amenielewa atasikia, otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na tulishakuwa tayari, hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani arusha juni 16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu ya mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa mgumu, ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"
Nassari.
Tumwombe Mungu ashike mioyo ya hawa wazee waliopewa dhamana ya kutuandia katiba,waandike kwa uzalendo wa hali ya juu,bila kuipendelea ccm rather katiba yakumlinda mtanzania na kumpa haki for the next 50yrs plus.Hapo tutapata di,qa ambayo haitampa mtu chama,kikundi cha watu kutawala nchi hii kama vle Mungu aliwapa wao tu kwa ajili ya matumbo yao wala c kwa watu wote.Binafsi namwomba Mungu ashike akili ya mzee warioba na mzee salum,wawe mazalendo kupita uzalendo,wawaachie watanzania katiba ambayo kila tutakapoisoma tubaki kuwabariki kwa urithi mzuri walioacha kwa watanzania na cio chama chao.katiba ambayo wananch watachagua viongozi wakuwaongoza,na cio mtu mmoja tu anapewa madaraka ya kumchagua anae mtaka yeye kwa maslahi binafsi,au ya chama au yakikundi flani nk.katiba ambayo kila mtu ataishi kwa kuhemu sheria hata kama ana pembe za chuma.Haya yoote mnayoyaona yanatokea ni matokeo ya katiba mbaya na utawala wa kamata fulani kwakuwa akichwa hv chama kitaumia,watu flani wataumia,maslahi yataingiliwa nk.Pia ndgu zangu wapinzani tunawapenda na kweli mmeleta changamoto nyingi mpaka ccm manajaribu kujikagua na kuamka usingizini walimokuwa.Lkn na nyie muwe na kiasi na pale pakufwata sheria fwateni sheria ili atakae kuja kukuonea basi tuweze kuwasema.Na nyie polisi tunaamini kuwa sheria mnazijujua kdogo ingawa nyie c wana sheria,lkn PGO inamwongozo mzuri wa sheria zenu na utekelezaji wake,msitii tu maagizo yoyote yanayovuja mipaka yenu kwa maslahi ya mtu,chama kikundi nk.,bali tekelezeni majukumu kwa haki na kwa mujibu wa sheria bila kujali chama cha mtu au dini au lolote.tumewapa dhamana yakulinda watanzania wote na mali zao c chama fulani na matakwa yao.God bless u all tuitakie amani Tanzania.
ReplyDelete