Izzo Bizness Aiponda TANESCO ... Asema "Ni AIBU ... "
0
April 13, 2013
Few minutes ago, rapper kutoka Mbeya City, Izzo Bizness ameonekana kukasirishwa na kinachoendelea katika Shirika La Usambazaji wa Umeme hapa Tanzania, TANESCO ...
Izzo ambae anafanya vyema kwa sasa na ngoma yake ya BALL PLAYER, ameonekana kuchukizwa sana na kitendo cha kukatika kwa Umeme kwa muda mrefu bila taarifa na pia kucheleweshwa kurudishwa ...
Izzo, "Tangu saa nane mchana mpaka sasa umeme hakuna halafu bila aibu eti mnasema kwa kujinadi #TumejaribuTumeweza Shame. " akionekana kumaanisha ni muda mrefu umepita toka umeme kukatika ...
Lakini aliongeza kuwa, kukatika huku kunarudisha nyuma mambo mengi ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na mawasiliano maana kwa muda wote huu uliokatika hata simu pia zinaisha charge na watu kushindwa kuwasiliana kwa kazi tofauti ...
Shirika la umeme limekuwa likilalamikiwa sana kwa tatizo lake la kukatika kwa umeme kwa miaka mingi huku kukiwa na dalili zote za kutoshughulikia suala hilo ...
Credits:GongaMX