Lady Jay Dee Asimulia Ndoto zake Mbili Alizoota Usiku...Help Needed


Kila ndoto naamini ina maana ila kwa bahati mbaya
Sio kila mtu ana uwezo wa kufahamu nini maana ya ndoto.
Naamini kila mtu huwa anaota
Ndoto zingine unazikumbuka ukiamka na nyingine huzikumbuki kabisaaa

Katika ndoto tunazoota huwa kuna
Mazuri, mabaya, dilema au hata vya kutisha.
 Nilipolala usiku wa kuamkia Jumatatu niliota ndoto tatu, mbili nilizikumbuka na moja niliisahau.

Naomba kusimulia ndoto zangu.

NDOTO 1:

Niliota nimejikuta mbele ya Nyumba ya mama wa mtu ninaemfahamu, Nyumba hiyo ilikuwa na kamba za kuanikia nguo, na nguo zikiwa zimeanikwa, mbele ya nyumba ya mama huyo pia kulikuwa na ndoo zimezagaa mbele ya nyumba na nyumba ilikuwa haijaisha kujengwa. (Pagale)
Mama wa mtu niliemuota sijazoeana nae zaidi ya salaaam.

Lakini mbele ya nyumba ya mama huyo nilikuwa nikiomba hifadhi usiku wa manane, bila kujua nilifikaje, wakati niko ndani  ya gari ndogo mfano wa Starlet.
Ambayo ilikuwa ni ndogo kuliko hata ndoo ya maji lakini sijui niliweza vipi kutosha ndani ya gari hiyo, niliendelea kupiga honi lakini hakuna alietoka wala sikuona mtu pembeni.

Zaidi ya mbwa wakubwa, weusi watatu, wakubwa kuliko hiyo gari.
Wakaanza kufoka na kushambulia gari kwa kung'ata matairi na kung'ata vioo
Walikuwa na nguvu kuliko mbwa wa kawaida niliopata kuwaona hapa duniani.

Mwisho mpaka nazinduka ni kwamba.
Sikung'atwa na wale mbwa, yule mama niliekuwa nampigia honi hakutoka kwenye ile nyumba
Na wala sikuona hata jirani yoyote kutoka labda kusema mwizi, mwizi
Na ndoto ikaisha nikazinduka, kama ilivyo kawaida ya ndoto hazifikagi mwisho.

NDOTO NO 2:

Kulikuwa na Gardner wawili, mmoja mrefu size ya Gardner wangu wa kawaida ninaeishi nae.
Mwingine mfupi na ana alama nyeusi kama mtu aliewekwa alama kutumia moto usoni.
Yule Gardner mfupi akaanza kugombana na mimi kwa kunishambulia kiasi cha mimi kushindwa kujitetea, alinishambulia sana kwa muda mrefu.
Gardner mrefu alipotokea akauchukua ule ugomvi wakaendelea kupambana
Sikujua ugomvi ulivyoendelea lakini ndoto ikaishia hapo.

NDOTO NO 3:
Bahati mbaya hii sikuikumbuka.

OMBI:
Ila napenda kufahamu kuna yeyote anaelewa maana ya ndoto hizi?? Na je! yupo pia anaeelewa maana ya kusahau ndoto.
Na unaipataje ndoto ulioiota ukaisahau, unaikumbukaje yani?

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mhhhh! we nae jiangalie maana siku hizi unapenda waganga waganga, sasa ndoto si ni ndoto tu. jiamini we ni mkristo bhana. kila mtu anaota na anaendelea na life sasa wewe ukiota iwe issue kwenda zako huko mfyuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sure mdau... Mara anajini mahaba???! Anaendekeza madawa oooohoo!! Km na ndoto kwako ni issue basi unatupa mashaka ww niwa aina gani.punguza ndumba la sivyo tegemea kuota mengi zaidi ya hayo...

      Delete
  2. Plz cc sio waganga!! Afu ww wa wanganga sn ndo maana sura yako nzitoooo.... Pesa zote ulizonazo lakini sura haichangamki??? Au we mganga??au...... Mmmmh... Now naanza kukuelewa...

    ReplyDelete
  3. Ndoto{1} kwa kifup ya kwanza ulikua umechukuliwa auponyumban kwako,na wale ulio waona sio mbwa ni fisi watu,4short} ndoto ya pili{2} kunajin mwanume ambaye anakusumbua {4shor}

    ReplyDelete
  4. mtabiri noumar hahahhahaha

    ReplyDelete
  5. **Toka umezaliwa mpaka kufikia umri huo umeshaota ndoto ngapi mpaka hizo ziwe special sana hadi kufikia kuomba tafsiri? Unakuolekea kubaya utafuga majini soon na utaishia kuwa mchawi kabisaa. Hao unaohisi ni waganga na kuwapa mwili wako wakaupiga chale ndio wanaokupandikizia midude ili uendelee kwenda kwako wakupige pesa tu.. **

    ReplyDelete
  6. Mfuate shekheh Yahaya akutabilie hzo ndoto zako

    ReplyDelete
  7. Pole sana dadangu! mimi huwa naota vibaya na nikiota mtu kafa anakufa kweli! mpaka najiogopa! ukiota ndoto mbaya amka na sali pia mkemee shetani na mambo yote mabaya! taja jina la YESU! kemea tena kwa sauti kubwa!! kila kitu kitakuwa sawa.

    ReplyDelete
  8. Kusali ndio njia ya kuepuka yote. Acha ushirikina mrudie YESU ndie jibu la matatizo yako. Ulikuwa mwanamke wa kuigwa ila cku zinavyosonga unapoteza mwelekeo its like ur so frastreted n dispressed. Focus!

    ReplyDelete
  9. Acha tabia za nebkadreza,waganga wako hawajakufahamisha?
    Acha kiburi na umrudie Mungu wa ukweli uliyemuacha,utakuwa salama.

    ReplyDelete
  10. Anayetupa tafsiri ya ndoto ni Roho mt,kupitia watumishi wake aliowapa karama hyo. Kwa kifupi maana ya ndoto zote mbili znafanana.
    1.gari huwa linawakilisha maisha ya mtu.
    2.mbwa ni mpepo ya ngono.
    3.gadner mfupi ni watu,maisha unayokutana nayo.
    4.gadner mkubwa ndio tegemeo lako

    5.mama uliyeomba msaada nakupiga honi hakutoka ni ishara kuwa unategmea watu na c Mungu.

    Therefore ulichoonyeshwa ni kuwa wewe unategemea watu,haswa gdner kuwa ndio msaada wako,bt hawatakusaidia kwa kuwa they ar merely human beings nt God,so amka na uanze kumtegemea Mungu.Thou hukungwatwa na wale mbwa,mapepo,ukiendelea kutumainia watu itakuwa halisi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad