Maskini:Kumbe Baadhi ya Waliofukiwa na Gorofa walikuwa Wakipiga Simu kwa Ndugu zao Kuomba Msaada mpaka zikaisha Chaji

Mke na watoto wafukiwa
Licha kwamba jengo hilo liliporomoka saa 2.30 asubuhi, baadhi ya watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa njia ya simu na wengine wakipiga kelele za kuomba msaada.

Idd Baka ambaye alikuwa akiwasiliana na mkewe ambaye aliegesha gari huku ndani kukiwa na watoto wake wawili alikwenda dukani kununua bidhaa, mara jengo hilo likaporomoka, alikuwa akiwasiliana nae hadi majira ya mchana simu ya mke wake haikuwa inapatikana.
Vifaa duni
Ni dhahiri kwamba endapo kungekuwapo na vifaa vya kutosha katika zoezi la uokoaji lingewezaa kufanikiwa kwa muda mfupi na kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapata majeruhi wakiwa hai.
Katapila latumika
Cha ajabu na aibu kwa taifa kutokuwa tayari kwa kuwa na vifaa vya kuokolea kwani tangu saa 2:30 hadi ilipofika saa 4.30 ndipo lilipatikana katapila moja ambalo nalo halikuwa na tija kutokana na kuwapo kwa uwezekano wa kuwakandamiza au kuwajeruhi zaidi watu waliofukiwa na kifusi hicho.

Kutokana na kutokuwepo na vifaa vya kukatia nongo waokoaji iliwachukua takribani dakika 15 kukata nondo zilizokuwa zimemkandamiza.

Umati wa watu ulivamia kifusi na kuanza kukisomba kwa mikono ili hali jambo hili lilikuwa kama mchezo wa kuigiza ambao umegharimu uhai wa watu zaidi ya 35 pamoja na kuharibu magari yaliyobondwa na kuwa kama chapati takribani matano.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. daaaaaaah!polen xana

    ReplyDelete
  2. hii ndo tanzaniaaa.

    ReplyDelete
  3. hii ndo tanzaniaaa.

    ReplyDelete
  4. m/mungu izilaze roho za marehem pepon Amin

    ReplyDelete
  5. m/mungu izilaze roho za marehem pepon Amin

    ReplyDelete
  6. Tanzania bwana noma,ingekua ni waheshimiwa ndo wamepatwa na janga vifaa vya uokoaji vingepatikana na kuletwa fasta eneo la tukio,ngombe wa maskini hazai,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad