Mume Apokea Kichapo cha Nguvu Kutoka kwa Mke wake Hadharani



Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.


Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali mwanamke huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na bwana wake huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana alikuja kishari na hata alivyokuwa akiongea na yule bwana wake tulibashiri kutokea kwa ugomvi.

“Kweli… haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai chanzo hicho.


Ikaelezwa kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo hilo.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad