Mwakifwamba Asema:Irene Uwoya ni Sikio la Kufa
0
April 12, 2013
RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Saimon Mwakifwamba amefungukia ishu ya msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni mke wa mtu, Irene Uwoya kunaswa hotelini na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusema mdada huyo ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa.
Akizungumza kwa uchungu na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema Uwoya hajitambui wala hajiheshimu kwani ni siku chache tu alirudiana na mumewe Hamad Ndikumana lakini inashangaza kunaswa akiwa na Diamond hotelini.
“Uwoya anatakiwa kujitambua kuwa ana nafasi gani katika jamii pia kwenye ndoa yake kwani maisha anayoishi siyo mazuri na yanatia aibu familia na tasnia nzima ya filamu hivyo abadilike,” alisema Mwakifwamba.