Akizungumza na Mwananchi katika makaburi ya
Kinondoni mara baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu na kuweka
mashada ya maua Mtegoa alisema yeye ni mkristo hivyo hana kinyongo na
mwigizaji huyo.
"Mimi ni mkristo tumeambiwa samehe mara saba
sabini, binafsi sina kinyongo chochote na ninampenda kama ilivyokuwa kwa
mwanangu, ila kila ninapomuona siachi kumkumbuka mwanangu," alisema
Mtegoa.
Alisema Kanumba alikuwa ni kama mtoto, mume, kaka
na kama rafiki yake, alimfanya kuwa mtu wa karibu yake na anashukuru
mwanaye pia alimfanya ajisikie furaha muda wote.
"Mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa ni Aprili 6
usiku, siku moja kabla ya kifo chake, tulizungumza mengi kwa njia ya
simu aliniahidi mengi na kunieleza kuhusu safari yake ya Marekani,
nammisi kwa kweli," alisema.
Akizungumzia suala ya ushiriki wake katika filamu
ya Without Daddy Mtegoa alisema "Nilikuwa naigiza tangu nasoma
sekondari lakini sanaa hapo nyuma haikulipa hivyo sikuendelea na sanaa,
baada ya kufariki Kanumba niliombwa nicheze filamu ya Without Daddy,
nilikubali na ikawa filamu yangu ya kwanza," alisema.
Alisema kwa sasa yeye anafanya kazi chini ya
Kampuni ya Kanumba The Great, hivyo itakapotokea filamu nyingine yupo
tayari kuicheza.
- Hatua za dharura kutumika kudhibiti dawa za kulevya Zanzibar
- TCRA yatangaza kiama wanaokiuka sheria ya mawasiliano
- SMZ yakiri kuathiriwa mabadiliko tabianchi
- Kutana na muuza dawa za kulevya aliyeishia kukatwa mkono, mguu
- Lipumba awashauri watu wa Tanga kufufua uchumi
- Bunge la Bajeti kuanza leo Dodoma
- CWT: Serikali inakaribisha mgomo mwingine
- Uhuru kuapishwa rasmi leo
- Mengi alaani vurugu za kidini
- Kagasheki aponda kauli ya Nchemba
- Mkapa atema cheche; ataka viongozi wafuate misingi ya Nyerere
- Chadema kuwasha moto bungeni
- CCM wamgeuka Waziri Kagasheki Loliondo
- Serikali yarudisha viboko shuleni
- Uhuru! Uhuru! Kesho ‘hakunaga’ Kenya
- Marekani yachelewesha kombora la masafa
- Kagasheki aponda kauli ya Nchemba
- Majengo ya Sekondari Ifunda yachomwa
- Dk Salim ataka Serikali kukomesha vurugu
- Wizara: Kagasheki hakualikwa mazishi ya Mawalla