Nani Wanamshauri Rais TZ?...Lazima Tutafakari Hili....Maana Nchi Hii ni Yetu Wote...


Katika nchi nyingi duniani...haswa zile zilizoendelea na ambazo nyingi tungependa kuiga mifano yao katika nyanja za kiutawala (mfano USA etc)..ni jambo la kawaida kwa marais wa nchi hizi kuwa na washauri (presidential advisors)katika nyanja mbalimbali.....mfano washauri wa kisiasa..au uchumi...au afya....au mazingira..n.k n.k....hii yote ikiwa na nia ya kumsaidia rais kuboresha maamuzi yake...ambayo ni kwa manufaa ya nchi nzima...na si chama chake au watu wake wa karibu..

Mara nyingi jopo la washauri wa rais kwa wenzetu hutoka kwenye highly professional think tanks....ambako wataalam waliobobea kwenye sekta husika hutumika na rais kumshauri.....hili wala halifanywi siri....na hamna msingi wa kulifanya siri......That said...tuje kwetu TZ...Nimeleta hii mada ili ijadiliwe (bila itikadi za watu kisiasa)kwa manufaa ya TZ...maana kupiga kelele mara nyingine kunasaidia....Kwa kweli kwa hali ilipofikia tz...kukemea ua kuhoji mambo ni lazima kabisa na ni haki ya kila mtanzania...maana hii nchi si ya chama wala mtu fulani..bali yetu wote...

Nimekua nikijiuliza sana naposikiliza hotuba za rais JK...kwa kweli mara nyingine nashindwa kupata majibu ya kwanini inakuwa hivi...Yaani kwa matatizo yaliyopo kwenye jamii ya tz sasa rais anapokuja na kuanza kutoa malalamiko kwa wananchi wake.....tena katika hali ya kuhuzunisha sana sana....wakati yeye ndie anatakiwa kuyashughulikia manung'uniko ya raia wake haingii akilini hata kidogo...Jibu pekee nililonalo ni kuwa rais JK hana washauri...na kama anao basi ni vihiyo....au washkaji wasio na uchungu na hali inavyoendelea hapa tz......

Kama sikosei...jambo la washauri wa rais kuwepo ni la msingi sana...na si siri hata kidogo katika nchi zenye maendeleo duniani....ni hapa kwetu tz pekee jambo hili wakati huu limekua siri kubwa...pasipo na msingi wowote...labda tujikumbushe tu huko nyuma...marais waliopita waliwahi kuwa na washauri kwenye mambo ya msingi kama uchumi....hata siasa.....namkumbuka mzee Mwinyi aliwahi kumtumia Prof.Lipumba kama mshauri wa uchumi....hata Nyerere alikuwa na washauri wake katika mambo fulani....na haikuwa siri....TZ ya sasa ina mabalaa chungu mzima...kuna migogoro ya kidini....matatizo ya ufisadi...siasa chafu..n.k..n.k...mambo haya yote yanahitaji umahiri mkubwa wa rais. kuyashughulikia....maana haya ni mambo ya kitaifa..na kwa maana hiyo haingili akilini hata kidogo kumwona rais anatoka hadharani na kulalamikia anaowaongoza....kama vile nchi haina kiongozi.....Kwa kweli kwa msingi huo lazima tuhoji nani wanamshauri rais nchi hii?...je wapo???na kama wapo wanafanya nini??...na kama wanafanya wajibu wao je wanasikilizwa??...kwa kweli lazima tujiulize...kwa hali ilivyo sasa TZ...

Kwa kuhitimisha..labda ifike sasa mahaliswala la rais kuwa na washauri iwekwe rasmi kwenye katiba yetu mpya...na mambo ya msingi ya kutolea ushauri kwa rais yaainishwe....yakiwemo maswala ya kisiasa....kidini....kiuchumi. .kiafya..n.k..n.k..

Source:Jamii Forums

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAPO MAPROFESA FEKI NA MADAKTARI WA FILOSOFIA FEKI WEWE UPO NCHI YAKO INAKWENDA KOMBO UNABAKIA KULALA NCHI ZILIZOENDELEA PROFESA ,DAKTARI WA FILOSOFIA ANGEKUWA ANATENGENEZA MITAMBO MIKUBWA ,ANASUKA MAGARI KWETU RASILIMALI TULIYYONAYO UMBEA ,UDAKU KUUZA SURA KWENYE LUNINGA KULALAMIKA TU HATUFIKI POPOTE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad