Ndege ya Marehemu Wakili Nyaga Mawalla yaanguka na kuharibika 'write-off'


Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha arusha.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina Babu Sambeke, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.

Taarifa zaidi zinasema kuwa hali ya rubani huyo si nzuri sana, na amekimbizwa kwenye hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.

Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.

UPDATE:
BOB SAMBEKE ALIYEKUWA RUBANI WA MAREHEMU WAKILI MAWALA. NYAGA NAYE KAFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acha uongo hiyo ndege c ya mawala na wala c ruban wa mawala..sambek mwenye ndo anaimiliki hiyo ndege...njo moshi ulizia babu sambeki uambiwe ni nani na ubilionea wake....

    ReplyDelete
  2. ni fedhehea kutoa taarifa bila kufanyia uchambuz!

    ReplyDelete
  3. izo ni propaganda za watu wasiomfahamu tu,mmiliki wa ndege izo babu sambeke

    ReplyDelete
  4. Acheni ujinga nyie mliocomment hapo juu, hamjui kitu ni bora mkae kimya tu!
    Sambeke alikuwa anamiliki ndege 1 tu ambayo ni 5H MXI ambayo bado ipo kiwanja cha ndege cha Arusha.
    Ndege aliyopata nayo ajali ni 5HQTT ambayo ni ya Mawalla.
    Msiongee kwa ushabiki tu wa kijinga kwa vile ni mchagga mwenzenu!

    ReplyDelete
  5. dah hiz blog zakikuz kichiz..mpekuzi ameonyesha ndege ya njano we umeonyesha nyeupe..haya bana cjui nan mkweli

    ReplyDelete
  6. sambeke anamiliki ndege,marehemu nyaga naye alikuwa ni mmiliki wa ndege kadhaa.Nyaga na Sambeke ni maswahiba wakubwa hata kwenye mazishi ya Nyaga alikuja pamoja na familia yake.R.I.P BABU SAMBEKE.

    ReplyDelete
  7. Mwone unavopenda kuparamia habari na wewe uonekane umo! Hufanyi uchunguzi unadaandia tu kupost,kwani lazima na ww uandike kwenye blog yako? Unabore kweli yani,yani ndo hasara za kupenda kukopi kopi kutoka kwa wenzako!ovyoo!

    ReplyDelete
  8. Isue hapa ni ajali ya ndege na waliohusika. Naona mnagombea Hati miliki sasa. Tumieni akili wakati wa ku ARGUE mambo.

    ReplyDelete
  9. We hapo juu unaelewa maana ya hati miliki?

    ReplyDelete
  10. eee muombeeni hata alazwe mahali pema pepon sio kubshana humu..
    R.I.P

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad