Producer Manecky Akana Kuvujisha Wimbo Mpya wa Diamond, Asema Diamond Huvujisha Nyimbo zake Mwenyewe
1
April 17, 2013
Producer wa AM Records Manecky amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwa studio yake na Diamond Platinumz kuwa walivujisha wimbo wake mpya ‘Mapenzi basi’ bila kumshirikisha msanii huyo.
Baada ya kupata maelezo ya Diamond jana akiiwalaumu producers wa AM Records kwa kuvujisha wimbo wake huo mpya na ‘Ukimwona’, leotainmenttz iliamua kumtafuta Maneck kwa kutumia muwakilishi wetu ili kupata maelezo yake kama mtayarishaji wa wimbo huo.
Manecky alianza kwa kusema kuwa yeye sio producer aliyeutengeneza wimbo huo bali ni mdogo wake anaeitwa Bob Maneck, na kwamba yeye hafahamu makubaliano kati ya Bob Maneck na Diamond kwa kuwa walifanya wimbo huo bila kumshirikisha yeye.
Alipoulizwa ni kwa nini nyimbo nyingi za Diamond anazofanya AM Records zinakuwa na matatizo yakiwemo kuvuja akafunguka,
“Nafanya kazi na wasanii wengi lakini kwa nini always nyimbo za Diamond tu ndo zinakuwa zinavuja, sasa we unadhani ni mimi au ni yeye ndiye anavujisha nyimbo zake, wewe kama ni mtu mzima na unaakili fikiria mara mbili halafu utalijua. Kwa sababu so far tunafanya project nyingi, Diamond kwani ni nani? Ni msanii kama wasanii wengine, tunafanya kazi na wasanii wengi kutoka nje na ndani ya Tanzania hii, lakini why always nyimbo zake ndo zinavuja. Sasa matatizo mengine sio yangu mimi ni yake yeye mwenyewe. Kwa sababu nyimbo tunazofanya lazima achukue anachukua demo.” Alisema Maneck.
Producer huyo ambae ni mshindi wa tuzo za Kili aliendelea kufuka na kutoa mfano hai wa kuvuja kwa wimbo wa Diamond ambao sasa hivi ni hit kuwa ilivujishwa na yeye mwenyewe na sio AM Records.
“ kwa mfano ile nini ‘moyo unanidundadunda’(Ukimwona) alichukua yeye mwenyewe demo, ushanielewa, imehit sawa maclub ina-bang ila ile ni demo, nyimbo ambayo haiko finalised, mimi ni producer nashangaa kuona nyimbo ni demo, kwani hamna music department za kuweza kujua hii nyimbo iko mixed au la? Lakini nyimbo zinabang!..sio kosa langu mimi ni lake yeye kwa sababu yeye anachukua demo,muda mwingine mimi nachukua blame ambazo yeye.... mbona hakuna msanii mwingine anayelalamika mimi natoa nyimbo zake, ni yeye tu kila siku WHY!aagrh..”
Diamond mkali ila tatizo anaulimbukeni wa vitu vingi tuna muhesabia days ajekuwa kama Mr nice.... Afanye afungue studio yake tuone kama zitakuwa hazi vuji
ReplyDelete