Takukuru ‘yazichonganisha’ Simba, Azam


Uamuzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwaachia huru wachezaji wanne wa Azam FC waliokuwa wakituhumiwa kupokea rushwa, umezaa mgogoro wa kisheria, huku Simba ikitaka Azam kuwalipa Sh1.8 bilioni kwa madai ya kuchafuliwa jina, jambo ambalo klabu hiyo ya Chamazi imegoma na kusema iko tayari kwenda mahakamani.

Mbali na kuitaka klabu hiyo ya Chamazi, Mbagala kulipa kiasi hicho, pia wanataka ndani ya siku saba kuombwa radhi na kinyume cha hapo watatangulia mahakamani kufungua kesi.

Takukuru ilifuta mashtaka ya wachezaji Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Deogratius Munishi na Said Mourad baada ya kukosekana ushahidi kuwa walipokea rushwa ya Sh7 milioni kutoka Simba ili wacheze chini ya kiwango katika mchezo wa kipigo cha mabao 3-1Akiwa Dodoma, Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage jana alitoa taarifa akiitaka Azam kutekeleza madai yao.

“Simba imeshawasiliana na wanasheria wake na uongozi wa Azam utatumiwa barua ya kutakiwa kutuomba radhi na wadau wake wote, pia kuilipa fidia ya Sh1.8 bilioni ndani ya muda wa siku saba,” alisema Rage. Rage alisema taarifa iliyotolewa awali na Azam kwenye vyombo vya habari ilikuwa katika lugha ambayo kimsingi ilishatoa hukumu dhidi ya Simba, jambo ambalo siyo la sahihi.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassoro Idrisa aliitaka Simba kuharakisha kwenda mahakamani kwa vile hawana mpango wa kuomba radhi wala kulipa fidia.
“Kama Simba inataka kwenda mahakamani ni sawa hatuwezi kuwazuia, ninachoweza kusema tupo tayari tukihitajika.

“Azam ina wanasheria, watakwenda mahakamani kupambana kisheria. Tuna hoja tutaziwasilisha, tutawasaidia Simba na tuko tayari,” alisema
Credits:Mwananchi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad