Unafikiri Sifa Kuwa na Kitambi? Sio Fashion Bali ni Ugonjwa


Mwenzenu nimekaa na kutafakari sana ndani ya moyo wangu na
na nimekuja na hiki kitu ambacho kimenishangaza na pengine kime-
nifanya niduwae sana, na wakati mwingine kimenifanya nione kioja
kwangu. Jambo ambalo limenifanya nilisema hapa ni kuhsu hawa
makaka, mababa, zetu jamani wengi wao siku hizi ukipishana nao
utasema alhamndulilahi Mungu amewaridhia sana na kuwakumbuka
yaani wengi wao siku hizi wana vitambi utafikiri wamebeba kila 50
za mahindi kwenye hilo tumbo, na wengine utaona wanavaa vishati
vya kuwabana ili kitambi kionekane, wengine wanadiriki kusema kuwa
ni fashion imeingia kwao. Jamani fashion hata kwa vitambi mm sijawahi
ona kabisa kuwa hata mwili nao ni fashion. 

Wao wanaona sifa kuwa na kitambi, eti kwao nifahari, wewe uliona wapi
kuwa na kakitambi ni fashion jamani, si maradhi hayo jamani, yani
unakaribisha maradhi mwenyewe mwilini mwako wewe nenda kwa
doctor akupime utaona kuwa kama huna kwashiakoo au utapiamlo
bandugu makaka, mababa zetu sio sifa kuwa na kitambi namna hiyo
kwani hata akina dada, mama, wanawake hawapendi mwanaume 
mwenye kitambi namna hiyo, atampeleka wapi mtu mwenye kitambi?
Mimi mwenyewe Ladyf sipendi kuwa na mume mwenye kitambi utafikiri
anaumwa utapiamlo, kumbe mwenyewe ni sifa tu na kusema yuko 
kwenye fashion, 

Wanaume nawasihi jamani punguzeni hizo tumbo zenu, fanyeni mazoezi
ya viungo, na fanyeni shughuli ambazo zitawapunguzia hizo mizigo ya
vitambi kwani kuwa na kitambi ni ugonjwa jamani. Maradhi mengine
tunayatafuta wenyewe kwa kula sana, yaani mwanaume wa siku hizi
bila kumsongea ugali unga 4kg hali anasema ni kidogo jamani mbona
mnatukondesha wake zenu hivyo. utafikiri unawapikia watu 10 hicho
chakula kumbe ni mmoja ndiye anayekula. Waungwana kaka zangu
wa jf acheni sifa ya kuwa na kitambi ni ugonjwa mnakaribisha.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanawake wa siku hiz wakiona mtu ana kitambi wanahisi atakuwa na maisha mazuri ndo maana wanaume wengi tunafuga vitambi,

    ReplyDelete
  2. mbona mnapenda kusingizia wanawake jamani, jisemeni wenyewe hamjui kutunza afya zenu na mnaendekeza mapombe na kula bila kiasi. tuacheni nasi wanawake tujiseme na yetu na si kututwika kila baya tunasababisha sisi....

    ReplyDelete
  3. Eti wanawake hahahahaha....makubwa...kwahiyo mnakula kwa sifa ili mfe mapema kisa ya wanawake....LMAOoooooo :))))))))))

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad