Wema Sepetu Aweka Picha Kuonyesha Alivyochunwa na Mama yake Baada ya Ugomvi
14
April 12, 2013
Picha aliyoweka Wema Sepetu Instagram kuelezea ugomvi uliotokea, na kuandika: ” Da fight I got into today caused me da marks I hav on my baq… things I do for da people I love always cost me… nd u knw wat ama kip doin.”
Staa huyo wa Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya Endless film, amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani nadani ya nyumba yake.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,”
Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
mmmm hayo matatzo gan mpaka umpeleke mother ki2oni..ingependeza matatzo yamalize kifamilia kuliko kuckia kuwa umemfikisha mama ki2oni...
ReplyDeleteakome nae,,,ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU
ReplyDeleteIla co ustarabu kumpeleka bimkubwa ki2oni haijaniingia akilini hy
ReplyDeletePesa zamzingua
ReplyDeleteMama yake naye kazidi uswahili. Kisa cha kumfuatilia binti yake na hali ameshakuwa mkubwa ni nini? Kama c kutafuta kudhalilika tu? Akae polic c ndo alichokitaka.....
ReplyDeleteNaomba mama huyu apewe hukumu inayo mfaa kwani tabia zake sio sawa Wema sio mtoto wa kuchapwa na familia kamwe
ReplyDeleteMi hivi karibuni nilisoma kuwa ndo msanii asiyejali kwa ayafanyanyo na kuandikwa gazetini/mitandaoni kama hivi ni sawa ana mambo mazuri afanyayo kwa jamii ila kama hili linaukweli BASI AMEPOTEA na UJINGA WA MAWAZO....akae ajiilize nn maana ya mama then atautia upuuzi wake
ReplyDeleteNB;WEMA WEWE NI MAITI INAYOTEMBEA POPOTE WAWEZA ANGUKA MRUDIE MUNGU UKASAMEHEWE
HUO NI UCHIZI WA WEMA. MAMA NI MAMA HATAKAMA AKUPIGE MAKOFI, HUPASWI KURUDISHA. WEMA SHOULD RELEASE HER MOM AND SEEK FOR FORGIVNESS.
ReplyDeletehuyo mama anampigia nini na umalaya kamfundisha mwenyewe hizo ni laana walizopewa na mungu kwa kumuuza binti yake kwa watu wenye hela alitegemea nn
ReplyDeletemmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletesasa wema amelewa sifa,hajui nini maana ya mama.
ReplyDeletekupenda kupenda kwake kuwa kwenye magazeti kila siku kutamtokea puani.
hivi kweli ni sahihi mtu kumfikisha mama yake kituoni kisa kaadhibiwa? kuna kitu amekifanya ndiyo maana kaadhibiwa. lakini si busara alivyofanya Wema. mmh labda ndivyo alivyofunzwa hivyo you never know
ReplyDeletehuyo wema aombe radhi kwa mama yake hata kama alichapwa na mama yake pia aombe msamaha kwa kuwa mzazi ni Mungu wa duniani,
ReplyDeleteWEWE WEMA UNALALAMIKA KWAMBA UNAZONDWA NA DUNIA. SASA HESHIMA YAKO IKO WAPI NA KITU GANI KITAKUFANYA WATU WASIKUZONGE? UNAFIKA HATUA YA KUGOMBANA MAPAKA NA MAMAKO MZAZI SASA BARAKA ZITATOKA WAPI. BASI UTAISHIA KUANDIKWA KWENYE MAGAZETI NA HAYO NI MACHACHE MENGINE YANAKUJA. MAMA NI MAMA HATA KAMA NI KICHAA MMFUNIKE MAMAKO LABDA KAMA AKIWA MLOZI SAWA..... MRUDIE MUNGU JAMANI........
ReplyDelete