Salaam,
Imekuwa ni tabia ya viongozi waandamizi wa chama (CCM) na serikali ya
JMT, haswa mawaziri, na wabunge wa CCM, kupiga kelele pale waambiwapo
kwamba serikali yao haifanya lolote la maana toka iwe madarakani.
Msingi wa kuambiwa hivyo, utokana na aina ya rasilimali tulizo nazo, na
uwiano na maendeleo yaliyopatikana. Kwa rasilimali tulizo nazo tulipaswa
tuwe mbali zaidi ya Norway (wanaotegemea uvuvi wa samaki na mafuta),
mbali zaidi ya Korea ya Kusini (ambao kwa mlingano wa rasilimali za
asili, hata hawafui dafu mbele yetu) n.k.
Sasa eneo moja ambalo wana CCM na viongozi hao upigia kelele na kutaka
kusifiwa, ni juu ya ujenzi wa barabara. Wanadai serikali ya CCM imejenga
barabara za lami kilometa nyingi mno (tena sifa zaidi upewe rais wa
sasa, ambaye usifiwa kwamba katika kipindi chake, barabara za lami
zilizojengwa ni nyingi mno ukilinganisha zilizojengwa kwa jumla yote
chini ya marais watatu wa kabla yake).
Katika kupitiapitia makarabrasha mbalimbali, nikakutana na MKUKUTA 2;
ambao unasema kwamba moja ya mafanikio ya kuonekana ya MKUKUTA 1 (kati
ya 2005-2010) ni ujenzi (upandishaji hadhi) wa barabara za changarawe/kokote/vumbi na kuwa za lami za urefu wa kilomita 2,200. Hizi ni kati ya kilomita 86,472 za urefu za barabara zote zilizopo Tanzania. Na kati ya urefu wa barabara zote, ni jumla ya kilomita 6,700 tu ndizo zenye lami nchi nzima. Kwa maana nyingine, chini ya rais Kikwete, serikali imeweza kujenga kilomita za barabara zenye lami kwa asilimia 2.5 tu!
Na kwa maana nyingine, serikali chni ya rais Kikwete haijajenga
barabara za lami zenye urefu zaidi ya wale waliomtangulia pamoja; kwani
kati ya barabara zenye lami (6,700km), kilomita 4,500 (sawa na asilimia 5.2
za barabara za lami nchi nzima) zilikuwepo kabla ya uongozi wake. Na
kwa mapana zaidi toka tupate uhuru, serikali za CCM zimeweza kujenga barabara zenye lami kwa asilimia 7.75 tu!!
Sasa kwa hali hiyo kelele uwa ni za nini?!? Haya wanataka wasifiwe kwa jambo ambalo hata kwa asilimia 10 hawajalifikia?!? Hata zikifika asilimia 100, sifa za nini, wakati ndiyo jukumu la serikali kutumia kodi zetu kuleta maendeleo?!?
Watanzania tusipotoshwe kwa mafanikio hewa; na tujenge tabia ya kusoma
maandikio mbalimbali ya serikali, kwani humo serikali yenyewe ukiri
madhaifu mbalimbali ambayo hadharani uwa haiyasemi!!!