Hii imemtokea binamu yangu, akiwa University alikuwa na boyfriend,
mapenzi ya ujana na ahadi za kuona, ikatokea binamu alipata ujauzito,
akiamini yuko kwenye strong relationship, akamumbia jamaa. Du kusikia
habari hiyo jamaa aliomba mimba itolewe na wamalize shule, waanze kazi
ndio wafanye mipango ya ndoa. Binamu yangu hakutaka kuitoa ile mimba,
tumbo lilivyoanza kuonekana, basi wazazi wake ilibidi wamuulize,
aliwaieleza ilivyokuwa, baba yake ambae ni mjomba wangu alikuwa mkali
sana kwasababu binamu yangu kwa akili za darasani alijaliwa.
Wazazi waliamua kumsaidia mtoto wao, wakampa support yote, alijifungua
salama mtoto wa kiume, na wazazi walimchukua mtoto yule akiwa na miezi
mitatu, ili binti yao aendelee na masomo. Binamu yangu alimaliza shule
na matokeo mazuri sana, alipata kazi, akajiendeleza zaidi na shahada ya
uzamili. Hakupata bahati ya kuolewa lakini anamudu kumsomesha mtoto
wake katika shule nzuri tu, na maisha yake na mtoto wake ni mazuri sana.
Kijana alitoka kwenye familia nzito, zengwe lilivyotokea, wazazi
walimtafutia shule nchi za mbali, akakata mawasiliano na binamu yangu
kabisa. Dunia ni duara, amekutana na baba wa mtoto, alimaliza shule na
kuoa, yeye na mkewe wamebahatika kupata mabinti wawili, sasa kujua mtoto
wa kiume aliye nae ni yule wa binamu yangu tu, anamsumbua sana kutaka
mtoto wake, tena kwakuwa binamu yangu hana mume, anajiona anahaki ya
kwenda kwake saa yeyote ile. Mpeni ushauri binamu.
huyo ndg yako aache ufala
ReplyDeleteUshauri gani,mambo mengine ni kutumia common sense,akijilegeza imekula kwake na atakuwa fala sana
ReplyDeletemimi ushauri wangu ni huu mtoto ameshazaliwa na aliyemgaramia mtoto mpaka akakuwa ni wazazi wa binti kwa nini huyu anayeomba ushauri asiombe kwa wazazi wake ambao ndio wamemlelea huyo mtoto wakati binti yao akisoma hapa sijui imekakaaje hii au wazazi wa binti hawapo hai anyway mimi ushauri wangu ni huu baba ni baba tu siku zote haijalishi amemlea au vipi huyu mwenye kutaka mtoto wake alipe garama zoote kuanzia mtoto alipo zaliwa mpaka sasa akishalipa anaweza kumchukua mtotowake kwa maelewano lakini hili jambo liende mbele ya sheria maana sheri ni msumeno ni hayo tuasikubali amchukue kirahisi

ReplyDelete