Askari Wetu wa Kwanza Kufa DRC..Tuwe Wamoja.. M23 Wameshindwa Kabla ya Kuanza

BARAZA LA USALAMA

Hapo tarehe 28 Machi, Baraza la Usalama la UN kwa kauli moja lilipitisha Azimio 2098, ambalo lilisafisha njia kwa chombo cha kwanza cha kimataifa cha kikosi cha mashambulizi. Mamlaka ya kikosi hicho cha kuingilia kati, itakayoundwa na vikosi vya askari wa miguu kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji na Malawi, ni "kuwamalizia nguvu na kuwanyang'anya silaha M23, waasi wa Kongo na vikundi vyenye vya silaha vya wenyeji na vya kigeni huko mashariki ya DRC, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

KUWEWESEKA KWA M23
baada ya maamuzi hayo ya baraza kuu M23 walianza kuhaha ikiwemo kumuandikia barua rais na bunge letu tukufu wakionya tusishiriki oparesheni hiyo ya kurejesha amani ya mashariki mwa CONGO.
Katika barua ya tarehe 11 Aprili, na kutiwa saini na Bertrand Bisimwa alionya kwamba M23 itaishinda kikundi cha UN itakachoongozwa na jenerali wa Tanzania ( Brigedia jenerali James Mwakibolwa).
Cha ajabu Bisimwa na wenzake wamekuwa wakiitishia Tanzania tu! vitisho hivyo havielekezwi malawi, musumbiji wala SA!
Ukipitia Account ya twitter ya m23( https://twitter.com/m23congordc ) kila siku wanaishambulia kwa vitisho Tanzania huku wakimponda rais wetu Jakaya Kikwete kwa kukubali kupelaka askari CONGO. cha ajabu hawawatishi malawi wala SA! wanaiogopa TANZANIA?

MAANDAMANO MJINI GOMA

Siku moja kabla ya kufika kwa kikosi cha pili cha Tanzania (chakwanza kilenda kimya kimya) waasi wa M23 waliendesha kampeni kubwa sana ya kuhamasisha wananchi wa GOMA waandamane kupinga ujio wa askari wa Tanzania mjini GOMA, kiongozi wa siasa wa M23 akiongea na wakazi wa Kibumba na huku hutuba yake ikirushwa na redio inayomilikiwa na waasi na kusikika mjini GOMA aliwaasa wakazi wa GOMA wafanye maandamano makubwa siku vikosi vya TANZANIA vinawasili, lakini cha ajabu na tofauti na waaasi walivyo tegemea hakuna Mkongomani hata mmoja alie andamna! hii inaonyesha waasi hawa wamepoteza ushawishi wAllio kuwa nao hapo awali.

PROPAGANDA YA KUANGAMIZA WATUSI

Waasi wa M23 wamekuwa wakiendesha vita ya kisaikolojia ya kuvichonganisha vikosi vya UN na wakazi jimbo la kivu wenye asili ya kitusi. M23 wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara na kusambaza vipeperushi kuwa WATANZANIA wamekuja kumsaidia KABILA kuwa teketeza WATUSI (maauaji ya halaiki) kitu ambacho si kweli. kunawatusi wangapi wanaishi Tanzania? si tungeanza na hao kama ndio lengo!
ukiangalia timu ya utangulizi ICGLR ambayo hasa ripoti yake ndio ilitumika na AU na baadae baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kupeleka BRIGEDI yakuingila kati, timu ilikuwa na makamanda kutoka majeshi yote ya nchi za maziwa makuu zikiwemo nchi za Rwanda, Uganda, Congo, Burundi nk: ambao walienda goma mwezi wa tisa mwaka jana wakiongozwa BRG: MWAKIBOLWA , sasa kama lengo ni kuteketeza watusi Rwanda ingekubali wapi? hata mazoezi ya awali ya kupambana na vikundi hatarishi kwenye nchi za ukanda wa Africa mashariki yalifanyika RWANDA, The Command Post Exercise (CPX) mazoezi hayo yalipewa jina la "Ushirikiano Imara" na yaliongozwa na Brigedia jenerali James Mwakibolwa akisaidiana na Brig. Gen Jacques Musemakweri wa Rwanda. hili la kuanzamiza watusi ni kuweweseka kwa M23.
Kubwa zaidi azimio hili wakati linapitishwa RWANDA ilikuwa mujumbe wa baraza la kudumu wa baraza la usalama, ingekubalivipi kupitisha azimio la kwenda kuwaangamiza watusi?!

TUMEJIANDAA KUPOKEA HABARI MBAYA?

Watanzania wengi ni watu wa kulaumu, wengi wanasubiri baya litokee kwa askari wetu huko DRC baaasi waanze kulaumu! lakini huwezi kulaumu maana hiyo ni hukla yetu watanzania, nivema serikali ikaanza kutuandaa pia kufafafnua ni nini tunakwenda kufanya congo na MADHARA GANI YANAWEZA KUTOKEA.
Kubwa zaidi ni kuendesha semina kwa waandishi wetu wa habari, wandishi wengi wa habari wa Tanzania wanependa kuandika habari hata kama hazina maslahi kwa taifa, lakni huwezi kuwalaumu maana kizazi kile kilicho shiriki vita vya uganda leo takribani wote wamestaafu, kunahaja ya kufundisha uzalendo kwa waandishi wetu?

mfano mzuri ni MALAWI, wao kwa sasa kwenye mzozo wa ziwa nyasa waandishi wote na taifa kwaujumla bila kuzingatia vyama vyaao wala dini wako kwenye "state of union" mfano muandishi wa makala wa gazeti la nyasa timmes ( Malawi Nyasa Times - Malawi breaking news in Malawi ) Patricia Masinga kwenye makala yake ya tarehe 5 mwezi huu nawafananisha viongozi wa tanzania na Adolf hitler! akidai ni wapenda vita ndio maana wanag'ng'ania ziwa malawai (ziwa nyasa) pia Partricia anaandika kuwa tunag'ang'ania kwenda CONGO kwaajili mali iliyoo CONGO na tunang'ng'ania ziwa malawi kwakuwa chini yake yamegundulika mafuta na gesi! Patricia Masinga pia anadai watanzania hatuji kiingereza ndio maana tumeng'ng'ania tunaushahidi kumbe ushahidi unatumaliza lakini kwakuwa hatujui lugha tumeung'mg'ania! haya matusi makubwa lakinimedia zetu limyaaaa!
wala sijaona waandishi wa tanzania wakihangaika kutetea nchi yao juu ya hilo.
mhariri wa NYASA TIMES katika kile alicho kiita TAHARIRI MAALUM 28/2/2013 alidai kuwa kama TANZANIA tunataka nusu ya ziwa nyasa basi turudi kwenye win win situation yaani turudishe ardhi yoote iliyokuwa chini ya utawala wa MARAVI KINGDOM ambayo ilitawala eneo kubwa la kusini mwa Tanzania kabla ya kuja wakoloni ambapo MARAVI KINGDOM ilikuwa inapaka na bahari ya hindi!

M23
Muandishi alie na waasi wa 23 Diana Katabarwa ambae pia naendesha account yao ya twitter fb na blog yao ya CONGO DRC NEWS amekua akiandika mfululizo kuwa Tanzania nikwenda kupigana na M23 kitu ambacho sio kweli, mashariki mwa CONGO kwenye majimbo ya Kivu ya kusini na kivu ya kaskazini na jimbo la Maniema kuna zaidi ya vikundi 33 vinavyotakiwa kunyang'anwa silaha, nyaweka ramani na maeneo vilipo.

FIB haiendi upambana na m23 bali vikundi vyote mashariki mwa CONGO viwe vinaungwa mkono na serikali au vinaipinga srikali lazima vyote vinyang'ang'anwe silaha wafundishwe vizuri na wajiunge na jeshi la taifa lao la CONGO au wajigeuze kuwa vyama vya siasa badala ya washika mitutu kutesa wanawake na watoto.

ASKARI WETU WA KWANZA KUFA DRC

Najiuliza hivi siku askari wetu, kijanA, wetu, mpendwa kafariki kwenye uwanja wa mapambano huko CONGO, athari hapa nyumbani itakuwaje?
tutaanza kupiga kelele vijana warudi nyumbani? tutanza maandamano kushinikiza JWTZ wajitoe? magazeti je? yataandika vipi?
TUWE WAMOJA, TUWAOMBEE VIJANA WARUDI SALAMA
MUNGU IBARIKI AFRIKA

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad