Katika kuonesha kuwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile ‘Babu wa
Loliondo’ bado ana fedha baada ya kuzikusanya kutoka kwa wateja wake wa
huduma ya kikombe, hivi karibuni alinaswa ndani ya Benki ya NMB akipata
huduma.
Babu alibambwa ndani ya benki hiyo Tawi la Loliondo mkoani Manyara
akihudumiwa na mmoja wa wafanyakazi aliyefahamika kwa jina la Lembris
Lesion ambapo inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi ya kujiunga na huduma
mpya ya Jisevie.
Akiwa benki hapo, Babu alionekana akijaza fomu huku akiwa na begi ambalo
linashukiwa kuwa na fedha ndani yake ambapo baadhi ya watu waliokuwa
wakimpiga chabo hawakuonesha kumshangaa wakiamini bado ana mkwanja wa
kutosha kutokana na ile tiba ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi hivi
karibuni.
“Unajua Babu alipata pesa nyingi sana na bado anaendelea kuzikusanya,
kimsingi ana pesa ndefu benki,” alisema mmoja wa wateja aliyekuwa eneo
hilo. GPL
wewe nawe mwandishi acha udaku, c pesa zake zinakuhusu nini? Mwache babu wa wa2.
ReplyDeletemwachie babu na hela zake
ReplyDelete