Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cuf kuwa ni chama
cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni,
wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...
Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema
asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..
Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.
Hiki ni Kipande cha hutuba hiyo ambacho nimekitoa Jamii Forums:
"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake
za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja
na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni
kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza,
Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org)
kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki
ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada,
Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group
cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo
nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na
msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano
na chama cha Kiliberali kutoka Norway.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya
Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni
umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake
mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii,
ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”.
Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika
serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party
cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata
mrengo huo.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote
ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao
na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa
vikipokea kutoka kwenye nchi hizo "
BUNGENI: Vurugu zasababisha Bunge kuahirishwa hadi jioni.
5
May 30, 2013
Tags
Cuf wanachukia bila kufikiri kwa kina coz Wenje yuko bayana
ReplyDeleteHakuna jipya..
ReplyDeleteWanachukia nini,na sera zao zinaelekea kwenye ushoga,usagaji,useless party with hopeless leaders!
ReplyDeletewatanzania kuweni na upevu mkubwa wa kufikiri abari iliyo tolewa ipo sawa kabisa. ila wapokeaji awajapokea kwa umakini na wengi wenu watanzania mnapokelea jambo kwa ushabiki na sio nia ya kutaka kufahamu mm naelewa kwanini chadema wanasema hivi kila chama kina taratibu zake jiulizeni ni kwanini wamesema awajakurupuka kusema hivyo ni mada iliyo andaliwa kama aina ukweli basi aipo mbali na ukweli. naishi ulaya sasa ni zaidi ya miaka 5 ukitembelea baathi ya makumbusho vipo vitu vingi sana toka Tanzania wapo chura wa Shaba wametolewa Tanzania imeandikwa chura hawa asili yake ni Tanzania. je ulaya ni Tanzania? jiulizeni maswali hayo then achene ushabiki tafuteni kuelewa.
ReplyDeleteWENJE FANYAKAZI MAANA UKOMBOZI WA NCHI NI GHARAMA SANA,WATAKAZANA KUPINGA LAKINI WATA ELEWA BAADAYE NINI ULICHO KUWA UNAKISEMA!
ReplyDelete