Chris Brown amethibitisha kuwa ameachana tena na mpenzi wake Rihanna
Juzi Jumapili muimbaji huyo wa ‘Fine China’ alisherehekea birthday
yake ya kutimiza umri wa miaka 24 kwa kuangusha party za nguvu katika
majiji ya Las Vegas, New York na Los Angeles, na kuweka wazi kuwa yupo
single na anaweza kujirusha na wasichana wengi atakao licha ya kudai
bado anampenda Rihanna wanayeachana na kurudiana kila mara.
Rihanna – ambaye alidai kuwa alipanga surprise ya nguvu kwa Breezy,
hakuhudhuria party yoyote kati ya hizo kwakuwa alikuwa busy kuperform
kwenye ziara yake ya ‘Diamonds World Tour’ weekend hii.
Credits:Bongo 5
Chris Brown athibitisha hayupo tena na Rihanna
0
May 07, 2013
Tags