Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo.
Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.
“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”
Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.
Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba.
Credits:Bongo 5
Au nyie lina na barnaba mameneja wenu ni akina ruge na wenzake ambao wana bifu na jd? Acheni hizo bhana
ReplyDeletemkumbuke nanyinyi mtamhitaji oooh hooo haya nyi mbanieni.
ReplyDeleteukweli ni kwamba nyie mko chini clouds fm..mnafata maarisho yakina ruge na kusaga..mnaogopa kuxhuxhwa kimzik..
ReplyDeleteHahahaha dunia na vituko vyake kila kukicha
ReplyDeletehabari ndio hiyo watoto wa ruge hao na mtakufa maskini kutokana na ufinyu wenu wa mawazo
ReplyDeleteMnamuogp ruge nyinyi mbwa koko
ReplyDeleteSio ishu dada hata peke yako unalisongesha JOTO HASIRA kaza but tupo nyuma yako.
ReplyDeleteHuoNdo ukweli hao madogo wako chini ya ruge na kusaga so hawawezi kuungana na jide. But sio issue mama jide ww kiboko unaweza kuwakimbiza cc tupo tutakupa sapot mama!!
ReplyDelete