Wana Jamvi,
Siku ya tarehe 26 April 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa
Fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa
hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;
Nilisafiri kwa gari binafsi kutoka Dar kwenda Arusha tarehe 21 April
2013 na nilitarajia kurudi Dar Ijumaa ya tarehe 26 April 2013 kwa
kutumia ndege ya Fastjet iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 3:30 usiku.
Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za Fastjet ni kuripoti dakika 40
kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka Arusha na
nilifika KIA saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale
iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na
kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta
na Bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza
kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba
pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri
mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na
mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi
wa Fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule Bwana
alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote
anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati
tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka
tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini
akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa
ajili ya ndege ya Jumamosi asubuhi tarehe 27 April 2013.
Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata
hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na
kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa Fastjet hakurudi tena ofisini
pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu
wa kuhudhuria Dar Jumamosi tarehe 27 April 2013, nilianza kufanya
mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya Precision
Air iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 1:55 asubuhi kuelekea Dar. Bahati
nzuri nilimpata mwakilishi wa Precision Air pale uwanjani ambaye baada
ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo
sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa Tshs.
195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha
taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya Precision
kutoka kwenye ATM. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya
kutafuta hotel ikaanza. Nilipata Hotel na nililala karibu saa 6 usiku.
Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za Precision Air pale
Arusha ili kupanda shuttle kwenda KIA. Kufika tu, nikaambiwa tayari
shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda
KIA (Ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa
haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria
ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika Dar kwenye
saa 3:45 asubuhi Jumamosi. Wakati turuka pale KIA, ile ndege ya Fastjet
tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale
uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.
Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana Jamvi kwamba wakati mwingine
rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu
nilitaka ticket rahisi ya Fastjet (Tshs. 107,000) one way lakini matokeo
yake niliingia gharama zifuatazo;
1. Ticket ya Fastjet Tshs. 107,000
2. Taxi Arusha KIA x 3 Tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 Tshs. 50,000
4. Ticket ya Precision Tshs. 195,000
Jumla Tshs. 502,000
Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet
na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena
hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu
wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.
Tiba
Source:Jamii Forums
Pole sana mara nyingi makampuni Mengi huwa wanapenda kuajiri watu wasio na uzoefu ktk kazi husika hasa za hapa nyumbani, ilimradi wasitumie fedha nyingi ktk kuwalipa,ndiyo mana kuujuwana na undugu umekuwa mwinga sana. Na wao bila kujua ni kwakiasi gani ataiathiri kampuni,Kama hivi kwasasa siyo wewe tu kutotumia hizo ndege tena watu wanajua sasa how weak they are!.wanatutia aibu sana hawa sasa hapo angeluwa mzungu Wala lisingetokea.
ReplyDeleteKiukweli hata mimi ilishanitokea mkasa unaofanana na huo kwa ndege ya fastjet! hawana na hawajui customer service. mteja kwao ni bwege! Mara elfu 10 precision
ReplyDeleteDa pole sana kwakuspend a lot of cash,sio ubinadamu kabsaa
ReplyDeleteHao FastJet kwanza ndege yao mbovu ilishatugomea kuruka mara kadhaa.Sio ndege customer service yao 0 .pole sana mdau kwa yaliyo kukuta.
ReplyDeleteWe learn through mistake don't go there again!!!