Hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi.
Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara walicharuka!
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani.
Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)
Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao.
Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi.
Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia.
Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.
Hali ni Tete Mkoani Mtwara Haya Ndio yaliyojiri Siku ya leo
4
May 22, 2013
Tags
Tanzania ilikua nchi ua Amani ila sasa amani imeanza kutoweka kwa kuxhoma gari la wagonjwa moto sioni kama ni suluhisho la ges kubaki mtwara au kuchoma majengo moto tukumbuke tunao teseka ni sisi watu wa kima cha chini hapo mtwara akitokea mgonjwa anayehitaji kusafirishwa haraka kwenda hospitali nyingine tutatumia usafiri gani?kwa vibosile hawana shida hawalitumii gari hilo na wala hawatumii hospital hizo ni sisi walala hoi tunaotumia gari hilo sasa kwa hasira zetu tumelichoma moto nani atakae teseka kama sio wakina mama na watoto.
ReplyDeleteKuna vitu vingine tufikiri kabla ya kutenda kwani hasira siku zote ni hasara Naipenda nchi yangu na Mungu ibariki Tanzania na watu wake mkiamua kufanya jambo fikirini kwanza faida na hasara zake shule,hospitali nivitu mihimu sana kwa jamii ukiviteketeza unategemea nini au ndio litakua suluhisho la gas kubaki Mtwara?Tuamke wana Mtwara.
Gesi haiozi tengenezeni sera kwanza wana mtwara kazeni buti msije mkatiwa mchanga wa macho kama wasukuma na madini yao
ReplyDeletewana mtwara sisi ndio tutakao pata shida na sio wanasiasa wanaotushauri kufanya hivyo fikiria kesho utapataje huduma usikae kuwaza mandamano wala vurugu utaumia wewe na mchochezi yupo kwake katulia anacheki matukio so usikubali kudanganywa amka kumekucha gesi ipo tu siku zote tafuta njia nyingine ya kuitaka gesi au bomba lijengwe mtwara wanasiasa wanatupoteza.
ReplyDeleteSiasa mchezo mchafu kuna raha gani sasa nyie wanasiasa kwa vurugu walizo fanya wana mtwara?nani anayeteseka nani aliyepoteza member wa familia?kama sio sisi tunaoishi Mtwara nyie mko mbali shida tunazipata sisi kwa uchu wenu wa madaraka.Hapa mtwara sasa hivi maduka,shule na hospital havifanyi kazi nina mgonjwa ndani siwezi kumpeleka kokote watoto wanalia njaa siwezi kwenda dukani hivi wakati mnawashauri hawa vijana kufanya fujo mlikuwa mnawafikiria akina mama wajawazito na watoto,vilema na wazee kweli?mko majumbani kwenu mnagogeaha glass kwa kusherehekea hamjui jinsi gani sisi wanamtwara tunavyoteseka.Kwanini msitafute njia nyingine ya kujijenga kisiasa kuliko hizi vurugu mnazo ziazisha.
ReplyDelete