Pamoja na kwamba alidumu wiki moja tu kwenye shindano la mwaka jana la
Big Brother Africa Stargame, aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania mwaka
jana, Julio Batalia bado ana mapenzi mazito na shindano hilo kiasi cha
kuachia wimbo, Mr Big Brother.
“Madhumuni ya kutoa single hii ni kuwakilisha Tanzania na muziki wetu
Africa na dunia, na pia nchi zenye kupendelea kuangalia Big Brother
ambao wafuatiliaji wa kipindi hicho cha miezi mitatu wako zaidi ya
million 20, amesema Julio kwenye maelezo yake.
“Huu ndo muda nchi yetu itasikika kirahisi kimuziki kwa nchi 54
Africa kwasababu ya nyimbo kuwa kali na vigezo vyote na kwamba
inahusiana na hiyo show. Wimbo unaitwa MR BIGB ROTHER na unaoongelea Big
Brother kama show,nchi zinazoshiriki,msiba tuliopata mwaka jana
heshima kutoka kwa watanzania baada ya kumpoteza mshiriki mkubwa mwaka
jana Goldie,” amesisitiza Julio.
“Huu ndio mwimbo wetu kwa mara ya kwanza katika historia ya
bigbrother msanii kutoka nchini kutoa mwimbo kwa ajili ya Big brother
Africa na support ya watanzania itatufanya kufikisha muziki wetu nje ya
Tanzania na Africa. Big Brother mwaka huu inaanza baada ya wiki mbili,
26 May. Tujivunie cha kwetu na kupeperusha bendera yetu Africa.”
Ngoma hii imetayarishwa na Timewreckordz na NK Production.Mpaka sasa
Julio ameshafanya ngoma na wasanii kama Chege, Matonya, Cassim,
Countryboy,Chidi Benz, Ukeme, Bskillz,Lamar,Lucci da don,Jokate,ROBZ na
wengine.