Jana nimebahatika kuisikiliza vyema taarifa fupi (KUNTU) iliyotolewa
na mlezi wetu mkuu wa kiroho KARDINALI) ya kuujulisha umma ni nini
kilichotokea kupitia chombo chake cha habari TUMAINI. Tunashukuru kwa
taarifa yake hiyo ambayo kwa jinsi ilivyotolewa, nina hakika ilifanyiwa
kazi ya kina kabla ya kuletwa hadharani.
Kwanza kabisa nashawishika kwa ukurasa wa awali kukubaliana na taarifa
yake hiyo kutokana na imani yangu kuu kwake, na inavyojulikana kwa
wachache kuwa kada ya UPAPA na UKARDINALI ni kada ambazo wanaozifikia
pia wamepitia mambo ya kiintelijensia!
Tunashawishika kuamini hivyo kutokana na jinsi kiongozi huyu wa kiroho
ambavyo ameweza kutoa ripoti yake ya kiintrijensia ndani ya chini ya
masaa 24! Amesema suala hili lisihusishwe kwa aina yoyote ile na dini au
itikadi ya uislamu bali waliofanya kitendo hicho ni WAKRISTO tena wa
KANISANI hapo! Na kwa msisitizo akasema kuwa anao uhakika wa kile
anachokisema!
Sasa inamaana kwa uweza wa kimungu ambao mtumishi huyu anao na ule wa
uintelijensia alionao ameweza kuwasaidia hata polisi wetu kumaliza kazi
ya upelelezi katika muda mfupi sana! Sasa kuna haja gani ya kuleta tena
CIA? Na kama amesisitiza kuwa taarifa yake aliyoitoa ndiyo ya mwisho,
kuna haja gani ya kuwashikilia hao watu wengine, si yeye apelike hiyo
ripoti yake polisi ili kazi iwe fupi na amani irejee mioyoni mwa watu na
kukata vilimilimi vya watu wengine ambao wanataka kupata umaarufu
kupitia SAGA hilo?!
Lakini tukija katika upande wa pili, Je, hatuoni kuwa mtumishi wetu
huyu amewahi saaaaaaaaaaaaaaana kutoa ripoti yake hiyo ambayo inaonekana
kama hitimisho la SAGA lenyewe?!
Na, Je, kama itatokea ikaja kuapatikina ripoti nyingine tofauti na hii
tuliyoaminishwa na mtumishi wa mungu, Je, tutamwamini nani?
Maswali yapo mengi sana kuliko yale ya papo kwa papo ya Waziri mkuu,
lakini katika hili nafikiri TAFAKARI ya kina ilitakiwa ichukuliwe kabla
ya taarifa hii kutolewa.
TAFAKARI ZAIDI.
Hata wewe hujielewi.. Mara unasema unamwamini pengo.mara hujui wa kumwamini. Kama taarifa ana uhakika nayo akae nayo asubiri ili iweje?? Ukitaka ataje waislamu ama ndo angekuwa hajakosea kuiwasilisha mapema? Kama unamwamini mkuu wa kanisa katoliki nchini hukupaswa hata kuhoji uamuzi wake.
ReplyDeleteSawasawa kabisa ndugu huyu admin ndio walewale hana jipya zaidi ya uchochezi
DeleteKwa hiyo, ndo nyoka amejing'ata mkia mwenyewe???©ÂºÂªÂªÂªÂªÂªÂªh
ReplyDeleteYaan huyu jamaa ndo anasababisha matatizo zaidi ni bora ukatulia kwnz co kuropoka tu
ReplyDelete