Kiwewe cha CCM Kinaipaisha CHADEMA!


Nimekutana na hii Jamii Forums.....Je ni Kweli  Kiwewe cha CCM kinaipaisha CHADEMA!....Jisomehe mwenyewe Mdau alivyoichambua .......

"Kabla ya mazingaombwe ya CD ya Rwakatare hali ya
ndani ya Chadema ilikuwa haileweki, kumbuka ndiyo kwanza walikuwa wametoka kwenye suala la akina Shonza na watu makini wanaofuatilia duru za kisiasa nchini walikuwa bado wanapima suala hilo uzito wake na madhara yake kama yangetokea.

Ccm sijui kwa kutokuwa na mipango makini au kukurupuka, au kiwewe wakaingia na CD! Chadema sijui kwa umakini au kwa bahati wakalifanyia kazi vizuri sana. Kwanza Mbowe alilibeba vizuri sana kwenye mikutano ya kuzindua kanda, nakumbuka mikutano yake ya Mbeya na kanda ya ziwa alilieleza kwa hisia na kuwajaza watu hasira kwa kuwaaminsha kwamba Ccm inateka watu na kuwaumiza kiasi kile kwa faida za kisiasa.

Kiboko yao alikuwa ni Marando Mabere alipowaumbua watekaji, na kama kawaida yao Ccm wakaja na utetezi 'kipumbavu' eti kuingilia mawasiliano ya mtu ni kosa! Hivi huu ni upungufu wa umakini kiasi gani?????? Badala ya kuwaondoa watuhumiwa katika tope hili, eti kuingilia mawasiliano ya mtu ni kosa!!!!

Likafuata suala la kufukuzwa wabunge machachari wa Chadema bungeni, hili nalo kulikuwa na jinsi ya kulikwepa maana Spika wakati anasubiliwa awaondolee adhabu au kuikazia angekuja na kusema nimewasamehe na ninawaonya kwa kosa hilo. Angekuwa ameliuwa suala kisiasa, badala yake akakazia hukumu na vijana wakaingia mitaani wakaomba huruma ya wananchi na kweli wakaipata. Ukidadisi maoni ya watu wanasema baada ya kuua uhuru wa vyombo vya habari na mahakama sasa wameliua bunge.

Kiwewe kikaendelea kwa suala la Lema, ujinga, ujinga, ujinga juu ya ujinga!!!!

Chama hiki kina washauri? Washauri wenyewe ni kina Nape na Mwigulu? Kama ni hao chama kimefilisika kiasi hicho?
Akina Mangula na Kinana wanakuwa wapi wakati chama kinafanya makosa ya kijinga na kitoto namna hii?

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. waache wafe taratibu 2015 tunaanua Matanga.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad