Kuna mambo mawili yanaleta tafakari isiyo na ulinganifu japokuwa yaweza kuwa na mwelekeo unaofanana, ila kiuhalisia unakinzana.
Mosi, baada ya kutangazwa rasmi kuwa Tanzania itapeleka majeshi yake
Congo, waasi wa M23 wameitaka Tanzania isipeleke jeshi lake huko.
Kwanini M23 wanapinga sana Tanzania kuleka jeshi lake huko? Kwanini
kelele zao ni kubwa sana kwa Tanzania lakini wako kimya kwa mataifa
mengine? Je! Ni kwamba wanaiogopa Tanzania ama wanaionea huruma
Tanzania, kuna nini kati ya nchi hizi mbili?
Pili, pamoja na kukatazwa kwenda Congo na M23, kwanini Tanzania
tunang'ang'ania kupeleka jeshi huko? Pamoja na hali ngumu ya kiuchumi
tuliyonayo watanzania kwanini Nshodha na Membe wanasisitiza jeshi letu
kwenda huko? Ok, mtu aweza kusema kwasababu Rais alikubali kupeleka
jeshi. Je kwanini Rais akubali kirahisi kupeleka jeshi Congo wakati
suala kulitoa jeshi nje ya mipaka yako ni suala lenye kuhitaji tafakari
kubwa zaidi?
Kwanini Tanzania inang'ang'nia kwenda Kupigana Congo (DRC)?
5
May 11, 2013
Tags
Binafsi naona ni upuuzi usio wa kumithirika, TZ tuna matatizo kibao yanayotushinda kuyatatua sasa iweje tukayatatue ya jirani tena kwa kuweka rehani roho za walinda amani wetu? Iweje tunaingilia uongomvi wa wana ndugu? Sitaki kuamini km TZ tunaviongozi wenye upeo mzuri wa kufikiri. Benard umepewa nini mpaka umekomaa kuwatoa sadaka wajeda wetu?
ReplyDeleteHapo kuna kitu,
ReplyDeletelkn amani ni bora kuliko mali
Hatuendi kupigana tunaenda kulinda amani kama wakitaka vita zana tunazo juzi juzi rais wa china alizileta havijawahi kufanyiwa majaribio
ReplyDeleteWewe...???
DeleteRaia basi vichwa vigumuuuu kama mbata,,hii issue ni ya umajo wa mataifa,,sio ya kikwete na M23,,fuckoff hamujui kituu
ReplyDelete