Hii imetoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu hii inaonyesha
ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyooko chini ya Dr John Pombe
Magufuli.
Mheshimiwa Spika,baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi
bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi
bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge
kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na
kifungu hiki alisema, naomba kunukuu “malipo ya madeni ya mwaka wa
nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi
usiohalisi hs.252,975,000,000.
Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya
madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba
hii sio halisi” (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98)
Mheshimiwa Spika,fedha hizi “zilizopotea”au “kulipwa kifungu hewa” ni
sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara ifuatazo kwa mwaka
huu wa fedha 2013/2014;
i. Barabara
ya Usagara-Geita-Kyamyorwa
(KM 422)
ii. Barabara
ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza-
Kaliua-Tabora (KM 443)
iii. Barabara
ya Nangurukuru-Mbwemkulu
(KM 95)
iv. Barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga
Port (KM 112)
v. Barabara
ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264)
vi. Barabara
ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda
(KM 359)
vii. Barabara
ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi-
Londo-Lumecha/Songea(KM-
396)
viii. Kuondoa
msongamano barabara za Dar
(KM- 102.15)
Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita
316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita
moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane
(800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka
Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya –
Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu –Goba (KM 9), zimepotea
kutokana na ufisadi huu.
Chanzo: hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa msaada Marcossy Albane.
Source:JF