Mainda:Baada ya Kubadili Dini yeye na Biblia, Biblia na yeye

MSANII wa filamu ambaye alikuwa Muislam na baadaye kuamua kuingia kwenye Ukristo na kuokoka, Ruth Suka ‘Mainda’ sasa anaonekana kupambana vilivyo kuhakikisha anaiboresha imani yake kwa kutembea na Biblia kila anakoenda.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Mainda aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa msanii huyo anaonekana kuwa na uchu wa kuijua vilivyo Biblia

“Kwa kweli sasa hivi Mainda hakaukiwi na Biblia mkononi, yeye na Biblia kila wakati. Kuna wakati hata akiwa lokesheni, akipata muda kidogo anaitoa na kuanza kuipitia. Hakika amebadilika,” kilisema chanzo hicho huku maneno hayo yakishibishwa na picha alizotupia Mainda kwenye mtandao wake wa Facebook zikimuonesha akiwa ameshikilia kitabu hicho kitakatifu.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. vipi kabadili dini bila kuisoma bila kuijua hiyo biblia inasema nini...hakuw mwiislamu wa kweli wa jina tu..nashauri aisome vizuri hiyo biblia itamludisha alikoto..nashangaa mtu kumkataa Baba yake nakumkubali babu..uislamu ni Baba wa vitabu vyote vilivyo pita...ili uwe mwiislamu sahihi lazima uamini vitabu vinne..1)torati 2)zaburi 3)Injiri 4)Qurani tukufu ukiviamini vitabu hivi wewe ni mwiislamu sasahihi.

    ReplyDelete
  2. uislamu daima hauhitaji watu ila watu ndo wanahitajia..ukitaka ufuate kwa maslahi yako ukitaka kufuru...hiyo ni hiyari yako jukumu la uislamu sio kuwalazimisha watu waingie ktk uislamu...ila jukumu kubwa la mitume wote waliopita nikuwafikishia ujumbe wa mwnyezi mungu au muongozo wa maisha kwa jinzi anavyotaka Mungu ili ufanikiwe hapa duniani na kesho peponi inakulazimu uufuate mwongozo huo..sasa kama huu ndo mwongo wa uislamu na dini zote zilizo pita..nataka aniambie huyo dada kipi kilicho mvutia ktk ukirsto?

    ReplyDelete
  3. Biblia ndo kitabu cha kwanza kuandikwa hivi vingine hakuna jipya. BIBLE ni Basic Instructions Before Leaving the Eath. Nampongeza dada kwa kumfuata Mungu alipo, hujapotea dada karibu sana, hata wakisema sana kumbuka nao wamezaliwa kama wewe, wataonja mauti kama wewe na mahakama yetu ni moja.

    ReplyDelete
  4. let the truth the known unto the world

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad