Mzazi mwenzangu kapata mwanamume mwingine akiwa chuoni/masomoni

Wakuu I really need ushauri wenu kwenye hili.: Nilipokuwa chuo kikuu third year nilimpa ujauzito girlfriend wangu aliyekuwa anamaliza kidato cha nne. Alijifungua like ten days kabla hajasafiri kwenda kidato cha tano alikopangiwa, wakati huo ndo kwanza namaliza chuo na kurudi nyumbani. So nikabaki na mtoto, nikimlea tangu hapo, na bahati nzuri nikapata kibarua kilichoniwezesha kumudu kumlea mtoto pamoja na kulipa ada ya shule ya mama yake.

Tulienda hivyo, wakati pekee wa yeye kumuona mtoto ni likizo za mwezi mmoja mmoja hadi miwili kati na mwisho wa mihula ya shule hadi alipomaliza form six (gharama zoote za masomo zilikuwa juu yangu), and nikawa nikiishi naye wakati akisubiri majibu ya mtihani. Kwenye mahusiano huwa hakukosi migongano ya hapa na pale na kwa kweli tulikuwa tukishindana katika masuala mbalimbali now and then, but tukawa tukisulihisha na maisha yanasonga. Bahati nzuri akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu so still nikabaki na mtoto akaenda chuoni (still nikawa nagharamia masomo yake kwa kila kitu, na bahati nzuri akapata mkopo kutoka Loan Board, so ikawa ahueni kwangu kwani nikawa najazia tu ile percentage ndogo inayobaki). Hapo sasa ndo mabalaa yakaanza kuibuka. Alipofika mwaka wa pili (ambao ndo yuko sasa hivi) kiburi na dharau vikazidi sana nikajua hapa lazima kuna jambo na si dogo. baada ya kumdadisi sana akakiri yeye ana mahusiano na mwanaume mwingine, and since maisha yangu na yeye yametawaliwa na kutoelewana kwingi, ameamua kusonga mbele na kamwe hatarudiana na mimi kamwe.

Na kweli ameshikilia msimamo wako barabara kwani nimejaribu sana kuomba arudi nyumbani tulee mtoto wetu bila mafanikio. Amedai huyo mpenzi wake mpya yuko mwaka wa m wisho (wa tatu) na eti wanapendana sana. Nimeamua kuangalia mbele na kuanza upya mkakati wa kuanzisha familia, though najua nimetoka naye mbali (5 years) and nilidevote resources zangu nyingi kuhakikisha anasoma vizuri. Any advice kutoka kwenu? niendelee kumng'ang'ania kama hali yenyewe iko hivi? Zipi ni haki zangu kama baba wa mtoto ninayemlea (sababu amejaribu kumention habari za kutaka kumchukua mtoto - ana miaka minne sasa)

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ayo n maisha yako na uyo mama n mchaw wako so ninakushaul w angalia maisha yako na jins gan yatakuwa mepes juu majukum yako na ur young ili uweze kufikia malengo coz aya n maisha cha mcng mafanikio

    ReplyDelete
  2. Duh pole sana mdau kubwa hachana nae Wala hakupendi huyo tena,ukimlegezea hata huyo mtoto anaweza kusema wewe si baba yake.Huwo ni utoto tu kwanza hajuwi hata how life is,Lazima atakutafuta tena huyo jamaa wakimaliza shule atamtema tu.Jaribu kufanya maendeleo yako piga chini Yule hasiye elimika kwa wewe ndiyo kila kitu kwake hata bikra uwenda ukawa umeusika fanya yako kaka wapo Wengi tu.

    ReplyDelete
  3. Dunia nzima imebadilika lakini Africa wasichana wanakuwa na matatizo sana,hata wakija ulaya,wanabadilika,hata km alikuwa mlokole,au msabato,au mwislam,wanakuwa km hawana dini,hayo ,na tabia km hizo ndizo zinazo changia umaskini sana,afrika ,watu hawaangalii miaka 20,50 ijayo wanaangalia hapo miguuni tu,Mungu atusaidie .
    Achana nae na upime afya yako km wewe ni mzima achana nae,na uwe makini sana.hata ukijifanya unahuruma atakuletea magonjwa.

    ReplyDelete
  4. Achana naye huyo mpumbavu kabisaaaaa.....!pesa ulizomgaramikia jihesabie umemtolea mwanao m2 wangu.sisi wanawake sometimes 2najisahau,honestly sometimes we make most wrong decisions and mistake,songa mbele,ataishia kujuta tu maana malipo ni hapa hapa duniani mbeleni mahesabu.pigo linamsubiria,

    ReplyDelete
  5. ni tabia zao tamaa wameweka mbele sana AMINI MUNGU YUPO
    ONE DAY ATAFANYA KITU

    ReplyDelete
  6. Kaka sobga mbele achana na huyo mwenye tamaa za kunguru!! malipo si pengine ni hapahapa. gharama ulizopoteza kwake hesabu umetoa sadaka we songa tuuuuuu!!!

    ReplyDelete
  7. ndugu ackuumize kichwa kwakuwa ameamua mpe baraka zote na huyo bwana wake mpya,kikubwa lea kilichochako ndo faraja yako ipo cku atarudi?

    ReplyDelete
  8. Please check me 0787610326. seriously i need to advise you something. Please if you real need a help just call me.

    ReplyDelete
  9. Pole sana kaka na pole sana kwa yaliyokukuta. Umeonesha mfano mzuri sana wa kuigwa, kwa kuwa responsible maana kuna wanaume wengi sana katika dunia ya sasa ambao wanakimbia majukumu yao. Ila pia, usidhani kuwa you have an obligation kwa huyo dada kwasababu ulizaa naye. Ukimuendekeza na wewe utaingia kwenye hilo shimo hata kama intentions zako ni nzuri. Mwanaume kama wewe unatutia pia moyo wanawake ambao bado tunaamini kuna wanaume wenye mapenzi ya kweli na wanatimiza majukumu yao. Endelea kumlea mtoto na maisha yako, na muache huyo dada maana huwezi lazimisha mapenzi. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  10. Achananae fala uyo kwan ajui alitendalo we cha mferej "FANYA YAKO J£MBE"

    ReplyDelete
  11. Pole bhana hao ndo wanawake,mi nakushaur temana nae 2 anza maisha yako upya 2 yan.!

    ReplyDelete
  12. pole jembe! piga chini huyo bwege ameonyesha kuwa akumbuki alikotoka wala anakokwenda anaishi kwa wakati uliopo hajui vyuoni watu wanatomba alafu wanasepa,atakukumbuka ila hata akija kuomba msamaha baadae usikubali asije kukuletea maradhi comred wangu,ingawaje umekuwa nae muda mrefu na kisaikojia inakupa shida kumtoa kichwani jitahidi kumsahau na jitafutie kasichana kengine karembo jioree taratibu utajenga mapenzi mapya na utamsahau wa kwanza hata mie niliwai kumpenda sana dada mmoja akanisaliti ilinichukua muda kumsahau lakini taratibu nilimsahau na sasa nimeoa na hata nikimuona naona kawaida sana.jitahidi jembe kumsahau

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad