CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa
kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015. Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam (06-05-2013), Katibu Mkuu wa chama
hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015,
nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye
magazeti.
Dk.
Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa
kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.
“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa
hatupokei makapi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi
kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa,
tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.
“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea
nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo
tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na
mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.
Hapa ndipo ninapoipendea CHADEMA .Ama kweli CHADEMA ni chama cha demokrasia.Hongereni viongozi wa chama.
Nafasi za wagombea ubunge CHADEMA 2015 Kutangazwa magazetini
3
May 08, 2013
Tags
SAFI SANA CHADEMA DAIMA
ReplyDeleteSAFI SANA CHADEMA DAIMA
ReplyDeleteSAFI SANA CHADEMA DAIMA
ReplyDelete