Rais Obama anatarajiwa kuzitembelea Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani iliyotolewa na
Ubalozi wa nchi hiyo nchini, inasema Rais Obama atazuru Afrika kuanzia
Juni 26 hadi Julai 3, ikiwa ni moja ya sehemu ya kuimarika uhusiano
baina ya nchi yake na bara la Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mahadhi Juma alisema ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa
kuinufaisha Tanzania maeneo ya biashara na uchumi.
Rais Obama ambaye ana asili ya Kenya ambako
anatoka baba yake mzazi, baada ya kuchaguliwa kushika madaraka nchini
mwaka 2009, alimwalika Rais Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza kwenda
Marekani kujadiliana masuala mbalimbali.
Ziara yake ya kwanza kwa bara la Afrika aliifanya nchini Ghana ambako alihutubia Bunge.
Acha aje bwana hawa ndio viongozi bwana sio wakina Mugabe na wenzake
ReplyDeleteNi june bana umetudanganya
ReplyDelete