Profesa Jay akana kuumendea ubunge mwaka 2015

Mchawi wa rhymes, Profesa Jay amesema hakujiunga na CHADEMA ili mwaka 2015 awanie ubunge kama wengi wanavyodhani
Rapper huyo wa ‘Machozi, Jacho na Damu’ ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule, ameliambia gazeti la Mwananchi la leo kuwa amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kukisaidia chama katika changamoto za kuikomboa nchi.

“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango wa kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama ili kuyafikia malengo,” ameliambia gazeti hilo.

Ameliambia kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na amekuwa karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua kuingia rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa vijana.

“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa muda mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria kumkomboa msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani nipo sahihi katika uamuzi wangu.”

“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini haina maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi kinanifaa, lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati wowote chama kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli kila mtu anahaki ya kuchagua itikadi aipendayo lkn hapo umechemsha kaka,pole.

    ReplyDelete
  2. Amechemsha nni,we nawe bwege tu,ushasema ana haki,tatizo liko wapi? Yaani nyie CCM ishawala 0718...........pole wewe,manake unahitaji pampers.

    ReplyDelete
  3. alitaka aingie ccm iliande akaendeleze ufisadi,maana huko kufisidi nchi wao ccm imekuwa kwao ni jambo la kawaida

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad